PDA

View Full Version : CCM kidedea Busanda!

mwanakijiji
05-24-2009, 08:24 PM
Ka nzi ka kijiji kametua Busanda tangu jana, na taarifa za matokeo ya uchaguzi zimeanza kutiririka sasa hivi. Kura zimemalizwa karibu masaa matatu yaliyopita.

a. Chadema kama ilivyotabiriwa inaelekea kuchukua ushindi eneo la Katoro (mjini) kwa ushindi wa tsunami.

b. Waziri mmoja Mwangunga adaiwa kukutwa na shahada ambazo hazijatumika na haieleweki kwanini amekutwa nazo..

Ach-F
05-24-2009, 09:01 PM
Jamani hivi CCM wanafikiri watatuburuza hadi lini? Chama cha majambazi ndio kinakufa hivyo... ... ... Kwa heri Chi chi emu bye.

Ach-F
05-25-2009, 01:24 AM
Habari zinazoingia ni kwamba chi chi emu, Chama Cha Majambazi wameshinda huko Busanda, kisa wamegawa t-shirts na pombe kibao kutoka kwa wafadhili wao wakubwa ambao tonge lao lililo mdomoni linahusudiwa ati na wapinzani.

Watanzania wachache wataendelea kuwa watumwa wa hawa makuwadi hadi hapo watakapoweza kuutokomeza kwa kuupigania, kama wakati wa biashara hiyo (Utumwa) iliposhamiri enzi za akina Sayeed Said na Basheer na genge lake la wahuni walioweka kambi Zanzibar. Sasa watawala wetu waliopewa dhamana wanawasaliti wale wanaowawezesha kula kodi yao. Time will tell Jakaya and soon or later you will regret the consequences.

dickabudi
05-25-2009, 02:38 PM
Mwanakijij tunaomba taarifa rasmi na mshindi wa kiti cha ubunge Busanda na mgawanyo wa kura hili litayusaidia kujenga hoja si lugha za kejeli na matusi ninazoziona zinadharirisha website yetu

mwanakijiji
05-25-2009, 09:16 PM
CCM imeshinda Busanda, hilo halina ubishi. Kwamba nilitarajia Chadema kushinda hilo nalo halina ubishi nalo lilitegemea mambo kadhaa na mazingira fulani ya kisiasa (niliyoyaanisha huko nyuma).

CCM imeshinda Ubunge na kutetea jimbo lake kiukweli na kihalisia ilistahili kushinda jimbo hilo. Hata hivyo ukiangalia vizuri utaona kuwa CCM haijashinda kushawishi mioyo ya yawatu zaidi.

Mwaka 2005, vyama vitatu vilisimamisha wagombea Busanda. CCM iliibuka kwa ushindi wa asilimia 79.2 (61,868) waliofuatia ni CUF asilimia 16.8 (13,094) na Chadema asilimia 4 (3,107). Hii ina maana kuwa wapinzani walipata jumla ya kura 16,161.

Wapiga kura waliojiandikisha ni 125886.

Hii ina maana gani?

a. Katika uchaguzi huu mdogo chama kilicho "gain" ni Chadema. Kama tukichukulia wale walioipigia Chadema mwaka 2005 ndiyo wameipigia tena mwaka huu (3107) basi kura hizi zinasema zaidi. Matokeo yanasema chadema imepata kura 22,799. Hizi kura zimetoka wapi? Kama wale wote wa CUF ndio pia wameipigia Chadema ina maana bado Chadema wangepata kura 16,161 lakini ziko 22,799!

Hii ina maana kuwa kuna kura 6638 ambazo zimetoka mahali pengine.

b. Kwa vile kura za CCM ndiyo zimepungua kutoka 61,868 hadi 29,242 ni wazi kuwa CCM haikugain. Kwa maneno mengine, chama kilichokubalika zaidi ni Chadema na si CCM. Kukubalika huko kunaonekana kwenye takwimu.

c. Nilisema huko nyuma kuwa siri ya ushindi iko kwenye kujiandikisha na wale watakaojitokeza kupiga kura. Kilichotokea Busanda ndicho pia kilichotokea Kiteto. Wakati ule nilifanya observation hii hii. CCM haishindi kwa kukubalika zaidi bali kwa watu kutojitokeza kupiga kura. Kama watu wengi wangejitokeza kupiga kura hata kufikiria asilimia 60 hivi au karibu ya sabini na ongezeko la Chadema lingefuata mtiririko wa ongezeko tuliloliona hakuna shaka hata kidogo Chadema ingeibuka na ushindi.

d. CCM inajua siri hii; wanajua kwa sababu wao ni chama kikongwe kinachojua mikakati na utaalamu wa uchaguzi. CCM haikuhitaji kushawishi watu wengi wajitokeze kupiga kura; ilihitaji kuwashawishi wana CCM kukipigia kura! NI kwa sababu hiyo basi ushindi wa CCM umetokana na wana CCM wenyewe; kama itafanyika tathmini tutaona kuwa karibu asilimia 80 ya waliopigia kura CCM watakuwa ni wana CCM au watu ambao wana mapenzi na CCM (kitu ambacho kina mantiki).

e. Wapinzani bado hawajafika kwenye kutegemea wanachama; wanategemea watu wenye kuichukia CCM; Huu ni mkakati wa kushindwa. Zile kura karibu 6000 za ziada (ukiondoa za CUF na Chadema) ni kura za wana CCM ambao hawajaridhika na hali iliyopo au watu wengine ambao na wenyewe wameona waachague vinginevyo. Binafsi ninaamini Chadema wangekuwa makini wangewekeza mtaji wao kwenye hawa.

Sijui muda wote wa kampeni Chadema imepata wanachama wangapi wapya Busanda. Sijui katika mikutano yao ya kampeni walitoa mara ngapi nafasi kwa mtu kujiunga na chama chao na kwa kiasi gani waliwaalika watu siyo tu kuichagua Chadema wakati wa uchaguzi bali kukichagua kama chama chao. Bila kuwa na base ya wanachama huwezi kushinda chaguzi za namna hii.

Hivyo, ushindi wa CCM si wa kupuuzia wala kubeza hata kidogo; ni ushindi wa mzoefu wa siasa ni ushindi wa mtaalamu wa mikakati. CCM ni chama cha kisiasa na kinaelewa majukumu na malengo yake ambayo ni kutawala. Katika hili hawana shida kutumia mbinu zozote za kisiasa kujihakikishia ushindi.

Mshindi ni mshindi tu hata kama goli lake la ushindi limekuja kwa penati! CCM inastahili pongezi zote na wapinzani hususan Chadema wanastahili pongezi kubwa zaidi kwa kuonesha kuwa wanaweza kushindana. Lakini hilo peke yake halitoshi, anayepewa tuzo ni mshindi tu, kuwa namba mbili siyo sifa ya ushindi.

Nsaji Mpoki
05-26-2009, 11:43 AM
Mimi mtizamo wangu unaangalia zaidi kujitokeza kwa waliojiandikisha wahakikishe wanatumia haki yao ya kikatiba kujitokeza kupiga kura.Nimefuatilia hizi chaguzi ndogo kuanzia Tunduru,Kiteto,Tarime,Mbeya vijijini na hii ya Busanda.Wapiga kura wanaojitokeza kupiga kura huwa chini ya 50%.
Najiuliza kuwa labda hawajitokezi kwa kuwa wanaona ni worthless excercise au hawana imani na wagombea waliojitokeza?Mimi kwa upande wangu kuwa huo ni ujumbe tosha kuwa hilo zoezi halina maana kwa wapiga kura wa Kitanzania.Nafikiri kuwa ni wakati muafaka tutafute njia nyingine ya kuziba mapengo haya yanayojitokeza baada ya Uchaguzi mkuu kupita.
Lingine ni baadhi ya wapiga kura waliojiandikisha kukosa majina yao siku ya kupiga kura.Ni wakati muafaka sasa kwa kuwa tuna daftari la kudumu kwa nini orodha hiyo isitolewe mapema kwa wapiga kura wajue kama wamo au hawamo ili mda upatikane marekebisho yafanyike.
Vilevile mfumo Electoral Commission wa kutumia watumishi wa serikali ukome,maana utiifu wao huwa kwa muajiri.Nikiunganisha Report ya matumizi mabaya ya fedha ya umma kama inavyotolewa mara kwa mara na mkaguzi mkuu wa serikali,naona kuna mafungamano ya chama tawala CCM na wasimamizi wa chaguzi(Ma-DED).Natoa angalizo hili,kwa kufuata matokeo ya uchaguzi mdogo wa Tarime.Kufuatia matokeo ya Tarime chama tawala CCM kuanguka,Mkurugenzi Mtendaji ambaye ndie alikuwa msimamizi wa uchaguzi huo mdogo Tracius Kagenzi amefunguliwa jalada la kumchunguza kwa matumizi mabaya ya fedha za serikali kule halmashauri mojawapo ya mkoa wa Mtwara.Ni mashaka yangu kuwa chaguzi tutakazoendelea kushuhudia hila zitafanywa na wasimamizi kupendelea chama tawala.
Mimi naona ni wakati muafaka wasimamizi wa chaguzi wawe permanent na waajiriwe na Tume ya uchaguzi.Tukubali kubeba gharama za demokrasia huo ndio ukweli wenyewe!

Nsaji Mpoki
05-26-2009, 11:47 AM
Mimi mtizamo wangu unaangalia zaidi kujitokeza kwa waliojiandikisha wahakikishe wanatumia haki yao ya kikatiba kujitokeza kupiga kura.Nimefuatilia hizi chaguzi ndogo kuanzia Tunduru,Kiteto,Tarime,Mbeya vijijini na hii ya Busanda.Wapiga kura wanaojitokeza kupiga kura huwa chini ya 50%.
Najiuliza kuwa labda hawajitokezi kwa kuwa wanaona ni worthless excercise au hawana imani na wagombea waliojitokeza?Mimi kwa upande wangu kuwa huo ni ujumbe tosha kuwa hilo zoezi halina maana kwa wapiga kura wa Kitanzania.Nafikiri kuwa ni wakati muafaka tutafute njia nyingine ya kuziba mapengo haya yanayojitokeza baada ya Uchaguzi mkuu kupita.
Lingine ni baadhi ya wapiga kura waliojiandikisha kukosa majina yao siku ya kupiga kura.Ni wakati muafaka sasa kwa kuwa tuna daftari la kudumu kwa nini orodha hiyo isitolewe mapema kwa wapiga kura wajue kama wamo au hawamo ili mda upatikane marekebisho yafanyike.
Vilevile mfumo wa Electoral Commission wa kutumia watumishi wa serikali ukome,maana utiifu wao huwa kwa muajiri.Nikiunganisha Report ya matumizi mabaya ya fedha ya umma kama inavyotolewa mara kwa mara na mkaguzi mkuu wa serikali,naona kuna mafungamano ya chama tawala CCM na wasimamizi wa chaguzi(Ma-DED).Natoa angalizo hili,kwa kufuata matokeo ya uchaguzi mdogo wa Tarime.Kufuatia matokeo ya Tarime chama tawala CCM kuanguka,Mkurugenzi Mtendaji ambaye ndie alikuwa msimamizi wa uchaguzi huo mdogo Tracius Kagenzi amefunguliwa jalada la kumchunguza kwa matumizi mabaya ya fedha za serikali kule halmashauri mojawapo ya mkoa wa Mtwara.Ni mashaka yangu kuwa chaguzi tutakazoendelea kushuhudia hila zitafanywa na wasimamizi kupendelea chama tawala.
Mimi naona ni wakati muafaka wasimamizi wa chaguzi wawe permanent na waajiriwe na Tume ya uchaguzi.Tukubali kubeba gharama za demokrasia huo ndio ukweli wenyewe!

Fingigwe
05-26-2009, 05:22 PM
Mkuu Mwanakijiji

Uchambuzi wako ni mzuri; una mantiki. Lakini napishana na kigezo kimoja tu cha chama cha siasa kutegemea wanachama wake katika chaguzi. Tukiangalia nchi zilizoendelea au hata kwetu si wote wenye utashi wa kujiunga na vyama vya siasa. Watu kama mimi, ambao ni wengi, hatuna interest na uanachama wa chama chochote lakini tunafuatilia kwa karibu sana mwelekeo wa kisiasa na - tunapiga kura! Tunapenda uhuru wetu wa kuamua chama kipi kinatufaa kwa wakati uliopo na kipi kipewe indiketa.

Nafikiri tatizo ni namna ya kuwahamasisha watu wa aina hiyo kuondokana na uvivu na kutafsiri kero zao kwa vitendo kwenye sanduku la kura badala ya kuishia kuzomea au kuwa "wachambuzi wa siasa" vijiweni. Nisingependa kuona ushindi wa chama unategemea sana kura za wanachama kwani huko itakuwa ni kujenga siasa za ushabiki zaidi kuliko za kupima na kuzawadia utendaji wa vyama. Tunataka demokrasia yetu siku zote iwe ni ya kinyang'anyiro majimboni "battle ground constituencies".

Kwa upande huo, nawasifu CHADEMA kwa kutingisha uhakika ambao CCM siku zote ilikuwa nao katika chaguzi za majimbo. Ona tu nguvu iliyotumiwa na CCM Busanda. Ni dalili njema kwa demokrasia nchini. Ni kweli pia kwamba CHADEMA wanahitaji kuimarisha mikakati yao kama vile kuwaelimisha wananchi wanaopenda mwelekeo wao kuhakikisha (zaidi ya kuzomea) wanapiga kura na pia ujinga kama ule wa Mbeya (V) haujirudii.

Aidha, hatuwezi kukataa kuwa kuna vitendo vya ubabaishaji vinavyofanywa kuwakwamisha kupiga kura wananchi wasioonyesha mwelekeo kwa CCM kwa kuwatisha, kukusanya shahada, kutoa misaada ya danganya toto n.k. Itachukua muda kwa wananchi kutofautisha kati ya serikali na chama tawala. Lakini mwelekeo hadi sasa ni mzuri. Kwa hilo, CHADEMA, kwa udogo wao, wanastahili pongezi.

mwanakijiji
05-26-2009, 08:59 PM
Mkuu Mwanakijiji

Uchambuzi wako ni mzuri; una mantiki. Lakini napishana na kigezo kimoja tu cha chama cha siasa kutegemea wanachama wake katika chaguzi. Tukiangalia nchi zilizoendelea au hata kwetu si wote wenye utashi wa kujiunga na vyama vya siasa. Watu kama mimi, ambao ni wengi, hatuna interest na uanachama wa chama chochote lakini tunafuatilia kwa karibu sana mwelekeo wa kisiasa na - tunapiga kura! Tunapenda uhuru wetu wa kuamua chama kipi kinatufaa kwa wakati uliopo na kipi kipewe indiketa.

Hili ni kweli.

Nafikiri tatizo ni namna ya kuwahamasisha watu wa aina hiyo kuondokana na uvivu na kutafsiri kero zao kwa vitendo kwenye sanduku la kura badala ya kuishia kuzomea au kuwa "wachambuzi wa siasa" vijiweni. Nisingependa kuona ushindi wa chama unategemea sana kura za wanachama kwani huko itakuwa ni kujenga siasa za ushabiki zaidi kuliko za kupima na kuzawadia utendaji wa vyama. Tunataka demokrasia yetu siku zote iwe ni ya kinyang'anyiro majimboni "battle ground constituencies".

Kwa upande huo, nawasifu CHADEMA kwa kutingisha uhakika ambao CCM siku zote ilikuwa nao katika chaguzi za majimbo. Ona tu nguvu iliyotumiwa na CCM Busanda. Ni dalili njema kwa demokrasia nchini. Ni kweli pia kwamba CHADEMA wanahitaji kuimarisha mikakati yao kama vile kuwaelimisha wananchi wanaopenda mwelekeo wao kuhakikisha (zaidi ya kuzomea) wanapiga kura na pia ujinga kama ule wa Mbeya (V) haujirudii.j

Hapa umesema jambo moja zito; sasa hivi CCM ili ishinde inabidi itumie nguvu zaidi kuliko ilivyokuwa huko nyuma ambapo ushindi ulikuwa ni granted. Sasa hivi wakifanya mchezo wanaanguka.

Aidha, hatuwezi kukataa kuwa kuna vitendo vya ubabaishaji vinavyofanywa kuwakwamisha kupiga kura wananchi wasioonyesha mwelekeo kwa CCM kwa kuwatisha, kukusanya shahada, kutoa misaada ya danganya toto n.k. Itachukua muda kwa wananchi kutofautisha kati ya serikali na chama tawala. Lakini mwelekeo hadi sasa ni mzuri. Kwa hilo, CHADEMA, kwa udogo wao, wanastahili pongezi.

hili la waliojiandikisha ni lazima tufikirie jinsi ya kulishughulikia. Nadhani kuna nadharia potofu kwani takwimu wakati mwingine zinadanganya kama hazijawa adjusted to reflect uhalisia uliopo. Hivi waliojiandikisha kupiga kura walijiandikisha lini?

edo
05-26-2009, 10:16 PM
Wakuu, kuna hizi tetesi kwamba wanachokifanya CCM ni kununua shahada za wapiga kura hasa ambazo wana uhakika kwamba wenye nazo hawataipigia CCM. Kwa maana hiyo wale tu wenye kuipigia CCM ndiyo wanaojitokeza kwa wingi wakati wa kupiga kura wakati zile za wapinzani zinakuwa zimeshapunguzwa kwa namna hiyo. Kuna mchangiaji mmoja ameligusia hili hapo juu. Hili nalo linaweza kubaininishwa vipi ukweli wake? Au ndo hivi tunavyoshuhudia mathalani, kwamba wapiga kura waliojiandikisha ni 100,000 lakini wanaopiga kura ni 40,000? Hawa wengine 60,000 wanakuwa wamepotelea wapi? Sina hakika sana kama tatizo hapa ni la kitakwimu kwani tofauti ya wapiga kura inayojitokeza ni kubwa mno!

Huwa sipati jibu jinsi ambavyo unaweza kuona watu walivyojaa kwenye mkutano wa kampeni wa mtu kama mh. Mbowe kwa mfano, halafu baadae ukaja kusikia kura ambazo chadema inakuwa imepata. Inatia kichefu chefu.

mwanakijiji
05-26-2009, 11:30 PM
Unajua haya ya kununua kura mimi siyaamini kwani muda wote huu yaani hakuna hata mmoja aliyedakwa "live" akinunua kura?