mwanakijiji
05-27-2009, 07:32 PM
UJUMBE WA WAZI KWA MHE. EDWARD LOWASSA: “Uchaguzi ni wako”
Na. M. M. Mwanakijiji
Endapo aliyekuwa Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Edward Lowassa (CCM-Monduli) ataendelea na mwelekeo wake wa sasa wa kisiasa na mahusiano yake ya sasa ya kimkakati basi njozi zake za kuja kushiriki tena katika uongozi wa juu wa taifa letu zitakuwa zimefikia ukingoni bila kupiga kelele ya breki. Na endapo nitakachoandika hapa hatakipa uzito wake unaostahili naomba niwe wa kwanza kutanguliza habari mbaya kwake na wale wanaomuunga mkono kuwa atashindwa. He will lose.
Ninaandika kwa sababu kubwa tatu; kwanza ni kwa sababu ninaamini anapoteza muda kwa kuendelea na machungu ya matukio ya mwaka jana; pili, anapoteza kipaji chake cha uongozi kwa kukaa pembeni ya mijadala ya kitaifa na hivyo kuonekana yuko upande kinyume na maslahi ya taifa na tatu, ni kwa sababu naamini hakuna mtu mwingine anayeweza kumuambia kile nitakachomuambia hapa kwa heshima na taadhima kubwa. Wengine aidha wanamuonea soni, wanamuogopa au kwa namna fulani wanagwaya mbele yake.
Inaendelea...
http://www.mwanakijiji.com/images/stories/habari/other/ujumbekwalowassa.jpg