mwanakijiji
11-13-2008, 03:42 PM
BARUA YA WAZI KWA WAZIRI WA SHERIA NA KATIBA
Sisi wafanyakazi katika Idara ya Mahakama Kuu Tanzania, Mwanza, tunaleta malalamiko yetu kwako dhidi ya Msajili wa Mahakama ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Frederita Mugaya jinsi anavyotenda kazi kama kampuni yake binafsi.
Tumeleta kilio kwako kutokana na manyanyaso, ufisadi na matendo mengine ambayo yanafanywa na Msajili wa Mahakama Kuu ya Tanzania Mwanza ambayo yanaenda kinyume na maadili ya utendaji wa serikalini na mashirika ya umma nchini.
Tangu Msajili huyo apandishwe daraja kutoka Mahakama ya Hakimu Mfawidhi wa Wilaya ya Mwanza na kuhamishiwa katika Mahakama Kuu, Mwanza, amekuwa akitumia fedha za umma kwa ajili ya manufaa yake ikiwemo kulazimisha tenda za ukarabati wa baadhi ya maeneo katika jengo la Mahakama Kuu kwa kujiamulia kuchagua mkandarasi ambaye anamtaka katika kufanya kazi hiyo hata kama atakuwa amechaguliwa na Bodi ya Tenda kwa ajili ya kufanya kazi hiyo.
Kwa upande wa ukarabati, ilitolewa tenda ambapo maombi mengi yalitumwa kwa ajili ya matengenezo ya choo katika mahakama kuu ambapo kiasi cha shs.10,000,000 kilikuwa kimetengwa kwa ajili ya kazi hiyo.
Matokeo yake, mkandarasi ambaye alikuwa amepewa tenda hiyo, ambaye ni Kashele Contractors, alinyimwa tenda hiyo na badala yake kupewa mme wake kwa kutumia vibarua wa mitaani kufanya matengenezo ya choo hicho.
Matokeo yake, hadi sasa choo hicho hakifanyi kazi na wafanyakazi katika mahakama kuu tunalazimika kwenda kujisaidia nje ya mahakama katika vyoo vya kulipia kati ya shs.100 hadi 200 jambo ambalo pia linawagusa wateja ambao hufika katika mahakama kuu kwa ajili ya kusikiliza mashauri yao.
Aidha, Msajili huyo katika kutekeleza kulinda maslahi yake, alihama na watumishi kama vile dereva, mtunza fedha pamoja na afisa utumishi ambao humulindia maslahi yake.
Msajili huyo alinunua nyumba iliyoko maeneo ya Ghana, mtaa wa Makongoro, kitalu 100 kutoka kwa Bwana Justus Magesa kwa kiasi cha shs. millioni 60. Nyumba hiyo licha ya kuinunua, bado anadai kuwa ni mali ya Magesa Justus Magesa na kuna malipo yanalipwa ya shs.300,000 kila mwezi kwa ajili ya pango linalodaiwa kulipwa kwa ajili ya kumpangisha msajili huyo wa mahakama kupita kwa Bw. Justus Magesa.
Pia Msajili huyo wa Mahakama Bi. Frederita Mugaya huwa anatumia gari zake binafsi kunyweshea mafuta katika kituo cha kuuzia mafuta ya petroli cha Sasa Kazi kilichoko jijini hapa kwa kutumia LPO za serikali.
Aidha, msajili huyo mara nyingi amekuwa akitumia fedha za serikali kwa safari zake binafsi pamoja na familia na marafiki zake hususani nyingi za safari hizo ni kuelekea jijini Dar es Salaam na Arusha.
Msajili huyo aliidhinisha kiasi cha shs.300,000 na kumlipa aliyekuwa kamanda wa polisi mkoani Mwanza, Bw. Zelothe Stephen kwa sasa yuko mkoani Mbeya kwa safari yake binafsi kwenda Dar es Salaam kwa shughuli zake binafsi.
Mwezi Desemba, 2006, msajili huyo alipokea kiasi cha shs.millioni 6 alizopokelea kutoka duka la Furaha ya Watoto lililoko katika barabara ya U TURN kutoka kwa Mkurugenzi wa Kampuni ya Kusindika Minofu ya Samaki ya Vicfish ili atoe hukumu ya kumfunga Mkurugenzi wa Pamba Engineering, Bw. Paresh Kapoor katika mzozo uliokuwepo kati ya Kapoor na mfanyakazi wa Vicfish aliyedaiwa kutukanwa na Bw. Kapoor.
Bw. Kapoor kweli alifungwa gerezani Butimba kwa muda wa miezi mitano na baadaye kutoka kwa rufaa iliyosomwa na Jaji Mackanja wa Mahakama Kuu.
Fedha hizo zilipelekwa na Mfanyakazi katika kampuni ya Vicfish anayejulikana kwa jina la Bw. Zuberi ambaye ni Meneja wa Ugavi katika kiwanda hicho.
Ni matumaini yetu kama itaundwa tume huru ya kuchunguza tabia na mwenendo wa Msajili huyo, itabaini kuwa kuna ukweli ndani yake na tunaomba msajili huyo ahamishiwe mahali pengine kuliko kuendelea na kero tunayopata sasa hivi.
Ni sisi Wafanyakazi wa Mahakama Kuu.