mwanakijiji
05-30-2009, 09:31 AM
http://www.globalpublisherstz.com/uploads/posts/thumbs/1243580326_kabula3.jpg
(toka Global Publishers"
Staa wa sanaa za maigizo nchini, Miriam Jolwa ?Jini Kabula? amesema kuwa penzi lake kwa sasa lipo buheri wa afya kwa Mfalme wa TAKEU, Nice Lucas Mkenda ?Mr. Nice?...
Kabula alilonga na waandishi wetu mapema wiki hii kwamba moyo wake sasa ni baridi kutokana na penzi maridhawa ambalo analipata kutoka kwa Mzee wa Kidali Poo.
?Nampenda Mr. Nice kwa sababu ana ubinadamu na anajua mapenzi. Kwake nimefika na tuna malengo ya kufunga ndoa,? alisema Kabula ambaye ni mzazi mwenza wa Mkurugenzi wa Jumba la Dhahabu, Jumanne Kihangala ?Mr. Chuz?.
Kabula aliongeza kuwa ameangukia kwa Nice baada ya kuona picha haziendi na Chuz ambaye alimuelezea kama mtu ?mzinguaji? na asiyejua thamani ya moyo kimapenzi.
Alisema kuwa hivi sasa anajuta kuwa na uhusiano na Chuz kwa sababu amemharibia dira ya maisha yake.
?Unajua kabla ya kuanza uhusiano na Chuz tayari mimi na Nice tulikuwa ni wapenzi, lakini baadaye Chuz akaingilia katikati na kuharibu mapenzi yetu. Naamini sasa hivi tungekuwa mbali,? alisema Kabula.