PDA

View Full Version : News Alert: Kikwete amzawadia Mshirika wa RA na Mhusika wa EPA



mwanakijiji
06-03-2009, 10:58 PM
JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA
WIZARA YA FEDHA NA UCHUMI
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI

1. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Jakaya Mrisho
Kikwete amemteua Bw. Peter Efraim Mayunga Noni, kuwa
Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Rasilimali Tanzania (TIB) kuanzia
tarehe 27 Mei, 2009.

2. Hadi uteuzi wake Bwana Noni alikuwa Mkurugenzi wa Mipango,
Mikakati na Utendaji (Director of Strategic Planning and
Performance Review) katika Benki Kuu ya Tanzania.

3. Uteuzi huu ni kufuatia Bw. William A. Mlaki aliyekuwa Mkurugenzi
Mtendaji kustaafu utumishi wa umma kwa mujibu wa sheria.

TAARIFA HII IMETOLEWA NA MSEMAJI WA WIZARA YA FEDHA NA UCHUMI

edo
06-04-2009, 06:10 PM
Hivi ni kweli kwamba ukishaingia kwenye siasa hata Mungu wa imani yako unakuwa humuogopi?Je, tunapaswa kuamini kwamba siasa zinaambatana na fitina,uonevu,dharau na kejeli kwa wengine?Ni kweli katika kundi la watanzania wote hakuna mtu wa kufanya kazi hiyo zaidi ya huyo bwana?

Kwangu mimi hii ni dharau ya hali ya juu na kwa kweli kazi bado ni ngumu kwa watanzania kurekebisha mambo haya!!