View Full Version : Program Alert: "Tuongee Asubuhi" na Star TV
mwanakijiji
06-05-2009, 09:14 PM
Nasikia kesho kuna mgeni muhimu kwenye kipindi hicho cha "Tuongee Asubuhi" ambacho kinarushwa saa 1:30 asubuhi. Mgeni huyo aliyeko Tanzania na mwanasiasa wa siku nyingi nasikia ataunguruma kwenye kipindi hicho na nimeomba mtu akiweza anirekodie na mimi nisije kumiss. Kutokana na unyeti wa huyo mgeni kwa sasa jina lake nalishikilia hadi atakapotambulishwa na wenye TV wenyewe.
Kama zile za Kipepe tuhakikishe tuna "TVs"..!
mwanakijiji
06-08-2009, 09:01 AM
Siku ya Jumamosi nilialikwa kuwa mmoja wa wachangiaji katika kipindi cha "Tulonge Asubuhi" kinachorushwa na Star TV Jijini Mwanza. Mada kuu ilikuwa tulilojifunza kutokana na Uchaguzi mdogo wa Busanda. Wachangiaji wengine ambao nao walipata nafasi ya kuchangia kwenye onesho hilo la asubuhi ni pamoja na Erasto Tumbo (Chadema), na Amos Makalla (CCM) pamoja na wapiga simu wengine. Ni matumaini nitaendelea kupata nafasi kama hii ili kuendelea kuchochea mabadiliko ya kifikra ambayo mara zote hutangulia mabadiliko ya kura! Unaweza kuniandikia: mwanakijiji@mwanakijiji.com
Click this link to check it out:
http://mwanakijiji.podOmatic.com/entry/2009-06-07T21_55_01-07_00
- Mzee Mwanakijiji
Powered by vBulletin™ Version 4.0.2 Copyright © 2012 vBulletin Solutions, Inc. All rights reserved.