dickabudi
06-10-2009, 11:20 AM
APRILI 29 mwaka huu ndiyo siku rasmi ambayo ilitangazwa na Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC), kwamba itakuwa ni kuanza kwa kampeni za uchaguzi mdogo wa Jimbo la Busanda wilayani Geita mkoani Mwanza.
Uchaguzi huo ulikuwa wa kuziba pengo lililoachwa wazi na aliyekuwa mbunge wa jimbo hilo kupitia Chama Cha Mapinduzi(CCM), Faustine Rwilomba Kabuzi. Uchaguzi huo ulishirikisha jumla ya vyama vinne vya CUF, UDP, CHADEMA na CCM. Kila chama kilikuwa na lengo la kuhakikisha kwamba kinaeneza sera zake kwa wananchi ili endapo watazikubali, basi chama husika kiweze kupewa nafasi ya kuwawakilisha wananchi hao bungeni.
Shughuli hiyo ilianza kwa kila chama kufanya mbwembwe za aina yake, lakini mbwembwe zilitofautiana sana baina ya chama na chama wakati wote wa kampeni hizo. Lengo langu la kuandika makala haya ni kutaka kueleza moja ya mambo mengi, niliyoyaona kama kero kubwa wakati wote wa kampeni hizo.
Lakini kabla sijaanza kueleza, napenda kutahadharisha kwamba kama kuna mtu ambaye ataguswa, popote alipo anapaswa kukaa chini na kujiuliza mara mbili kulikoni.
Jambo lenyewe lililonikera sana kuliko yote, niliyoyashuhudia kwenye kampeni hizo, ni baadhi ya waandishi wa habari waliokwenda jimboni humo kuripoti habari za uchaguzi huo wa Busanda.
Kwa hakika waandishi hao, walifanya vitu ambavyo kwangu mimi naamini kwamba ni kinyume na maadili ya kazi hii ya uandishi. Sijui yawezekana wao vyuo walivyosoma maadili kama haya, yapo na yanapatikana kwa wingi. Ninacholenga kukizungumzia hapa, ambacho kwa hakika nimeona si vyema kukiacha kikapita hivi hivi bila kuwekwa hadharani ni baadhi ya mambo ya uongo, ambayo yaliandikwa na baadhi ya waandishi wa habari waliokuwepo katika kampeni hizo.
Moja ya vitu vikubwa vya uongo ni taarifa kwamba Makamu Mwenyekiti wa CCM (Bara), Pius Msekwa na Makamu Mwenyekiti mstaafu wa CCM (Bara), John Malecela, walizomewa katika moja ya mikutano ya kampeni za chama hicho katika kijiji cha Nyarugusu wilayani hapa. Wakati waandishi hao wakiandika hivyo, Msekwa alikuwa ameondoka jimboni humo siku moja kabla ya mkutano huo kwenda Afrika Kusini.
Kitu cha pili ni taarifa kwamba mkutano huo pamoja na mingine mingi ya chama hicho, ilikuwa ikizomewa na hasa mgombea wa CCM, Lolesia Bukwimba, ambaye mwisho wa siku aliibuka na ushindi. Nilichokishuhudia katika kampeni hizo mwanzo hadi mwisho ni kwa waandishi wa habari, ambao naweza kudiriki kusema kwamba walikuwa ni wa CHADEMA wakati wote wa kampeni hizo.
Walikuwa wakihudhuria mikutano ya CCM na hasa iliyokuwa ikifanyika Katoro, Lwamgasa, Bukoli na Nyarugusu na kisha kujitenga pembeni kabisa wakikaa karibu na kundi maalum la vijana, waliokuwa wakizomea mikutano ya CCM. Waandishi hao wapatao sita hivi, walikuwa wakifika kwenye mikutano ya CCM ambayo ilikuwa ikifanyika katika maeneo hayo niliyoyataja. Walikuwa wakikaa karibu kabisa na kundi hilo muda wote wa mikutano. Kwa mfano viongozi wa CCM wakisema ?CCM hoyee? wao walikuwa wakijibu ?Huwiiiiii?.? na baada ya hapo utawaona waandishi hao wakiinama na kuanza kuandika.
Lakini kibaya zaidi kuna wakati waandishi hao, walikuwa wakifikia hatua ya kuwapigia wahariri wao simu na kuwawekea simu ili wasikilize namna ambavyo kundi hilo lilikuwa likizomea kwa kupiga mayowe.
Naamini wahariri hao, nao waliamini kwamba jambo hilo lipo na ndiyo maana kila siku kwenye baadhi ya magazeti, yaliyopeleka waandishi wake, yaliibuka na habari za kuzomewa kwa CCM kwenye mkutano. Wahariri hao hawakuelewa kwamba walikuwa wakifanyiwa mchezo mchafu. Hakika kwa mara ya kwanza niliamini kwamba kumbe kuna baadhi ya waandishi wa habari wanaoandika uongo na kupika maneno. Huko nyuma niliamini kwamba waandishi wa habari huandika kweli tupu kwa kuelimisha, kuburudisha na kuikosoa jamii, lakini sasa hali siyo hivyo.
Hata hivyo, hatimaye matokeo kwa ajili ya uchaguzi mdogo wa ubunge wa jimbo la Busanda, yalitangazwa na mgombea wa CCM, Lolesia Bukwimba, akaibuka mshindi. Hili ni funzo kwa waandishi hao na vyombo vyao, ambao walilazimisha watu kuamini uongo wao. Naamini mtu ambaye alipata kusoma baadhi ya magazeti ya kila siku nchini, aliamini kuwa CHADEMA ingeweza kushindwa.
Katika uchaguzi huo, Lolesia alifanikiwa kuibuka kidedea dhidi ya wagombea Finias Magesa (CHADEMA), Oscar Ndalahwa (CUF) na Beatrice Lubambe (UDP). Mimi naamini wao na vyama vyao, waliweka zaidi maslahi binafsi mbele kuliko yale ya umma na ndiyo maana baada ya wananchi kugundua hilo waliamua kuviadhibu vyama hivyo.
Ushindi huo kwa mgombea wa CCM umepatikana baada ya kuvuka kipindi cha kampeni, ambacho kiliambatana na kila aina ya ?vituko?, ikiwemo baadhi ya wanasiasa kusema uongo na kuungwa mkono na vyombo vingi vya habari.
Kampeni hizo zilishuhudia ?vituko? ambavyo kwangu mimi naamini vinapaswa kukemewa, kwani hali hiyo ikiachwa iendelee, itafika wakati ambapo kutakuwa na uvunjifu wa amani, jambo ambalo si utamaduni wa Watanzania.
Serikali inatakiwa ivinyooshea kidole baadhi ya vyombo vya habari na waandishi wasiofuata maadili ya kazi hiyo, kwani walidiriki kudanganya umma, ama kwa habari au kwa picha, ambazo kwa kuziangalia kwa makini zilibainika zilikuwa za ?kutengeneza? au kubuni. Hivi kama unafanya kazi kwa misingi ya kufuata maadili unaweza kufanya vitu kama hivyo?
Ni bora waandishi hao wajitangaze wazi kwamba wao ni wafuasi wa CHADEMA, CUF ama UDP, kama ambavyo baadhi yao wametangaza na wanajulikana kwamba ni wafuasi wa chama tawala, CCM.
Hivi kuna haja gani ya kuvaa ngozi ya kondoo wakati ndani ni mbwa mwitu mkali, ambaye muda wote mdomo wake umeachama ukihitaji chakula?
Ipo mifano kadhaa kuhusu habari na picha hizo. Lakini, kwa uchache niseme hili kama ilivyokuwa habari ya Mei 15, mwaka huu, kuhusu madai ya kuzomewa kwa viongozi wa CCM. Habari hiyo ilifanana kila aya katika magazeti mawili ya kila siku, yaliyokuwa na waandishi wawili tofauti Busanda. Hiyo ni mbali na picha iliyoonyesha helikopta ikiwa juu ya vichwa vya watu, lakini maelezo yake yakiwa kuwa umati mkubwa wa wananchi walikuwa wakiishangilia ikitua.
Inashangaza na kuhuzunisha sana, kuona baadhi ya vyombo vya habari vikikubali kupindisha maadili, kwa sababu ambazo hazijajulikana. Hali hiyo iliwafanya watu kuhoji kama lengo lilikuwa kukidhi haja zao za kisiasa - kuona CCM inashindwa au ni kutokana na kuwepo kwa mazingira ya rushwa.
Naamini binafsi kwamba sheria haizuii wala kukataza chombo cha habari, kuunga mkono chama cha siasa, lakini kama kinataka kufanya hivyo, maadili yanaeleza kuwa kinapaswa kutangaza msimamo wake hadharani, kama inavyotokea katika nchi zilizoendelea.
Kama chombo cha habari kitakuwa kimetangaza hadharani kuunga mkono chama cha siasa na katika mkutano wao wakajitokeza wahuni wawili au watatu wakazomea wafuasi wa upande pinzani, kikasema watu wamezomewa au kikaonyesha helikopta ikiwa juu ya vichwa vya watu, hilo halitakuwa tatizo, kwa kuwa kitakuwa tayari kimetoa msimamo wa upande kinaoegemea.
Maana yangu hapa ni kwamba waandishi wanaojifanya hawana vyama, wakati ndani ya mioyo yao wana ushabiki na chama fulani, wanamkosea Mwenyezi Mungu na wananchi, kwa sababu wamefanya dhambi ya uongo.
Natoa tahadhari kwa vyama vyote vya siasa nchini, kuwa macho na waandishi kama hao, kwa sababu ipo siku vitawageuka na kwenda kuandika habari za vyama vingine. Ni bora vyama vya siasa vikawa wazi na kuwataka waandishi hao waonyeshe itikadi zao za vyama, kwa sababu yawezekana walionekana kukishangilia chama hicho baada ya kupewa vijisenti na kuwezeshwa chakula, malazi na mavazi. Lakini, pia magazeti nayo yajitokeze na kutangaza msimamo wake kwa chama na si kuwa ndumilakuwili. Huo ni uwendawazimu!
Ushindi wa mgombea wa CCM katika jimbo hilo, unaonyesha kuwa Watanzania ni werevu wa kutosha, kuweza kujua mbivu na mbichi.
CCM kwa kutumia viongozi na makada wake mahiri, wakiwemo Naibu Katibu Mkuu (Bara) George Mkuchika, John Malecela, Anne Kilango na John Magufuli, kilinadi sera na hatimaye wananchi wa Busanda wameonyesha kuzikubali na kumchagua mgombea wa CCM.
Viongozi hao, na wengine ambao sikuwataja, ni mfano wa kuigwa kwa kuwa wameonyesha umahiri wa kumwaga sera na kufafanua kuhusu utekelezaji wa Ilani ya Chama, badala ya kujikita kwenye matusi na vitisho, kama ilivyokuwa kwa viongozi wa vyama vingine, hasa Chadema.
Ushindi wa CCM katika jimbo la Busanda ni ishara tosha kuwa Watanzania wengi, kamwe hawawezi kudanganywa na kampeni chafu, zilizojaa hadaa na uongo wa kupindukia.
Viongozi wa upinzani na baadhi ya vyombo vya habari, wanapaswa kufahamu kuwa wananchi wanachotaka ni kutatuliwa kero zao na si umaarufu au uhodari wa mtu kutumia majukwaa. Wananchi wa Busanda wanafahamu jinsi serikali ya CCM, inavyojitahidi kushughulikia kero zao hatua kwa hatua ; na wamefanya uamuzi wao wa mwisho kwa kumpigia mgombea wa CCM. Tuheshimu uamuzi wao huo wa mwisho! Hiyo ndiyo demokrasia!