View Full Version : Dr. Kamala is wrong on Land Policy!
mwanakijiji
11-14-2008, 04:37 PM
Dr. Kamala speaking on behalf of Tanzanian government has said categorically that Tanzania's land policy would not be changed so as to allow foreigners (including our neighbors) to own land. According to his own words he told other EA ministers in Kampala recently that "we love you, and you are our friends, but Tanzanian land will be for Tanzanians".
If this is true then how can we have an economic integration or a possible political federation without harmonizing land policies in the region? Should the Tanzanian government modify its land policy so as to enable any East African to own land in the country?
I believe Dr. Kamala is wrong on this one.
Mpita Njia
11-14-2008, 06:17 PM
Nadhani si tatizo la Dk kamala, ni tatizo la serikali ya Tanzania. Mpaka sasa sijaona ikionyesha msimamo unaoeleweka katika hili. kamala anapokuwa anazungumza nje, kwenye furum ambako anabanwa na majirani zetu, huwa anatoa kauli ambazo zinaashiria kuwa suala hilo linajadilika. lakini akirudi hapa nyumbani, anaposikika kwa watanzania wengi, anatoa kauli kuonyesha kuwa suala la ardhi si sehemu ya makubaliano, nabaki nashangaa
Mpitanjia na Mwanakiji ninyi mawazo yenu katika hili ni yapi? Naona sijawaelewa vizuri, ninachokiona hapa ni misimamo isiyo na uhakika ya Bwana DR K na serikali.ninyi mnasemaje?
mwanakijiji
11-14-2008, 11:32 PM
Mpitanjia na Mwanakiji ninyi mawazo yenu katika hili ni yapi? Naona sijawaelewa vizuri, ninachokiona hapa ni misimamo isiyo na uhakika ya Bwana DR K na serikali.ninyi mnasemaje?
Mimi naamini katika mambo makubwa mawili:
a. Kama kweli tunataka ushirikiano wa kiuchumi tuweke mwelekeo katika kuunda shirikisho moja (nchi moja). Aidha tufanye hivyo au tusijariibu kufanya hivyo; haya mambo ya kuweka mguu mmoja majini na mwingine ardhini unaitwa Undumilakuwili.
b. Ardhi ni suala nyeti kwa Taifa lolote lile; Kama unataka ushirkiano na nchi nyingine huwezi kusema "tushirikiane hiki lakini hiki hapana" wakati hicho unachokatazia ni muhimu katika mahusiano yenu. Ni wazi kuwa kati ya nchi zote za AM Tanzania bado ina ardhi kubwa zaidi hivyo katika kujiunga ni lazima kuangalia ni kwa namna gani ardhi yetu inaweza pia kuwa yao.
Tunachotakiwa kufanya na kuendeleza ni kile Nyerere aliamua mapema kweli kuwa ardhi itabakia mikononi mwa serikali na Rais ndiyo atakuwa na dhamana ya kuishikilia ardhi na hivyo hakuna mtu anayeweza kuja na kusema "hii ni ardhi yangu". HIvyo Rais anaendelea kuwa na uwezo wa kufuta umiliki wowote wa ardhi kinyume na nchi nyingine kama Kenya na Zimbabwe ambapo ardhi ilikuwa inaweza kumilikiwa in perpertuity.
Suala la ardhi naamini siyo suala la kukataza tu bali ni suala la kuja na sera nzuri kwa mwekezaji, lakini pia ni nzuri kabisa kwa mwananchi wa Tanzania.
deny_all
11-15-2008, 03:00 PM
Nadhani Dr. Kamala kikubwa alichogusia ni kuwa kati ya nchi zote tano, Kenya, Uganda, Rwanda, Tanzania & Burundi ni Tanzania peke yake ndio inaonekana itakuwa mtoaji wa ardhi hizi nchi nyingine hazina cha kutoa kwa hali ilivyo sasa.
Tunachotakiwa kufanya na kuendeleza ni kile Nyerere aliamua mapema kweli kuwa ardhi itabakia mikononi mwa serikali na Rais ndiyo atakuwa na dhamana ya kuishikilia ardhi na hivyo hakuna mtu anayeweza kuja na kusema "hii ni ardhi yangu". HIvyo Rais anaendelea kuwa na uwezo wa kufuta umiliki wowote wa ardhi kinyume na nchi nyingine kama Kenya na Zimbabwe ambapo ardhi ilikuwa inaweza kumilikiwa in perpertuity
Kwenye nchi za wenzetu nadhani sera ni tofauti, mtu anamiliki ardhi milele na milele generation & generation ni mali yake. Kwa maana hiyo ni rahisi zaidi kwa sisi kufuata jinsi umiliki ulivyo kwa nchi kama Kenya kuliko kusema sheria zibadilke Kenya, serikali ndio imiliki ardhi.
Suala la ardhi naamini siyo suala la kukataza tu bali ni suala la kuja na sera nzuri kwa mwekezaji, lakini pia ni nzuri kabisa kwa mwananchi wa Tanzania
Hili nadhani limeshazungumzwa wazi kuwa wawekezaji makini wakija na hela na mipango ardhi wanapatiwa. Nadhani mifano hai, umeshasikia wawekezaji wanaokuja kutaka kulima mazao kwa ajili ya biofuels ( soma hapa (http://www.sunbiofuels.co.uk/content/projects-tanzania) )
Mpita Njia
11-16-2008, 12:08 PM
Mpitanjia na Mwanakiji ninyi mawazo yenu katika hili ni yapi? Naona sijawaelewa vizuri, ninachokiona hapa ni misimamo isiyo na uhakika ya Bwana DR K na serikali.ninyi mnasemaje?
Katika mazingira tuliyomo, mimi siamini kabisa katika aina ya ushirikiano tunaotaka kujenga. Tunafanya makosa kutumia muungano wa Ulaya kama mfano tukisahau kuwa Ulaya wameungana huku wanachama wengi (at least wale wa mwanzo) walikuwa na nguvu ya kiuchumi-walichounganisha ni nguvu zao.
Sisi hapa unaweza kusema ni wagonjwa, uchumi na hali zetu ni dhooflhali. Siamini kuwa ukiunganisha wagonjwa watano, unaweza kumpata mtu mmoja mzima, hata kidogo.
Tubaki kama tulivyo, kila mmoja kivyake, tukiweza kuimarisha chumi zetu, hapo ndipo tuungane na utaona katika mazingira ambayo kila mmoja ana nguvu, huu wasi wasi unaoonekana hivi sasa kwamba kuna walio na dhamira ya kutaka kuwameza wengine, hautakuwepo
Ach-F
11-16-2008, 11:43 PM
Kenyans wameshindwa kuchukua ardhi yao kutoka mikononi mwa wachache na wanafikiri wanaweza kuja Tanzania na kujipatia ardhi bwelele. Kwanza ni lazima wakome na hata wakipewa atakapoingia Obama wetu madarakani atawafukuza. Hivi wanafikiri Tanzania ni wajinga? Wameshindwa kukaa kwa amani nchini kwao na sasa wananyemelea kama fisi aliyeona mfupa. Rwanda - Kagame anashirikiana na M7 kuendeleza mauaji Congo Watanzania ni lazima tukae chonjo saa mbaya.
Kama Kenyans wameshindwa kukaa kwa amani na majirani wao kwa ukabila na kuuana kama kuku wanaweza kweli kuishi na sisi? Pengine wengine hawafuatilii yale yaliyotokea baada ya uchaguzi lakini niseme hivi kuna raia wa Kenya ambao wamehama miji na makazi yao ati kwa sababu sio wa kabila walikoenda kujenga na kufanya biashara.
Powered by vBulletin™ Version 4.0.2 Copyright © 2012 vBulletin Solutions, Inc. All rights reserved.