PDA

View Full Version : CUF - kulikoni?



Mpita Njia
06-12-2009, 11:44 AM
Katika mlolongo wa matukio, kubwa linalozungumzwa hivi sasa kuwahusu ni kujiuzulu kwa Wilfred Lwakatare kutoka kwenye nyadhifa zote alizonazo isipokuwa uanachama wa kawaida.
Lakini kwa wafuatiliaji wa mambo, hasa ya siasa, wanafahamu fika kuwa kuna msukosuko (hata kama ni wa chinichini) unaonedelea ndani ya Chama cha wananchi (CUF). Wenyewe CUF wanaweza kupinga hili kisiasa lakini ndai ya mioyo yao wanajua kuwa hilo lipo.
Mimi binafsi bado nakichukulia chama hiki cha upinzani kama kielelezo cha chama ambacho kimeoneysha kwa vitendo jinsi ambavyo siasa zinapaswa kuendeshwa. Najua kuwa wana makosa yao ya hapa na pale na naamini hilo ni jambo la kawaida.
Kinachonishangaza ni kuwa yanayotokea hivi sasa ndani ya chama hiki yanaonyesha kuporomoka kwa kasi na kwa kiwango kikubwa kwa chama ambacho uimara wake ulikuwa ni tishio kubwa kwa CCM. najua zipo sababu kadhaa zilizowahi kuanishwa, lakini siamini kwua ndizo hasa zinazosababisha mtikisiko mkubwa kiasi hiki ndani ya CUF kwa sababu hata viongozi walizijua na kutokana na utaalamu wao katika siasa, isingewawea vigumu kuzidhibiti.
Kwa nini viongozi wameshindwa kudhibiti hali hiyo kiasi kwamba chama hiki kinaonekana kipo hatarini?
Kuna lolote amballo CUF walitakiwa kulifanya, wakashindwa kulifanya au ambalo hawakutakiwa kulifanya na wao wakalifanya?
Najua kwua wengi wanaamini kuwa kujiuzulu kwa Lwakatare ambako kunaweza kuishia kwenye kujiondoa kabisa kwenye chama hicho, hautakuwa mwisho wa CUF, lakini je, huo hauwezi kuwa ndio mwanzo wa mwisho wa chama hicho?

serengetibaridi
06-12-2009, 02:10 PM
Viongozo wakongwe wa chama hicho kwa sasa wamechoka. Wamedumu kwa muda mrefu sana hivyo sera zao sio update. wawachie wengine waongoze chama hicho. Lasivyo kinakoelekea ni Kaputi

Mpita Njia
06-12-2009, 02:34 PM
Viongozo wakongwe wa chama hicho kwa sasa wamechoka. Wamedumu kwa muda mrefu sana hivyo sera zao sio update. wawachie wengine waongoze chama hicho. Lasivyo kinakoelekea ni Kaputi

Sasa hapa kiini cha tatizo ni nini? Viongozi (watu), mawazi ya viongozi hao? Au mfumo ambao CUF bado inautumia kujiendesha kama chjama. Kuna uwezekano kwua viongozi si tatizo bali mfumo unaotumika. Lakini pia nawezekana pia kuwa mfumo uliopo ni mzuri lakini viongozi waliopo hawana uwezo wa kuutumia mfumo huo kwa ubunifu wa kukiendeleza chama

mwanakijiji
06-13-2009, 12:43 AM
Nafikiri kuna zaidi yakile ambacho tunakisoma kwenye magazeti. Nilimsikia Lipumba akielezea kuwa kujiuzulu kwa Lwakatare si mgogoro wa aina yoyote na hakuna matatizo yoyote baina ya uongozi na Lwakatare. Hata hivyo, maneno ninayoyasikia leo ni tofauti sana.

nyemela
06-17-2009, 06:44 PM
Nina Imani Pro. Lipumba ni kiongozi mzuri na anaweza kuipeleka CUF mbali lakini amekosa wasaidizi wazuri. Kuondoka kwa Lwakatare kuchukuliwe kama challenge na uongozi wa CUF ili kuweza kukijenga upya chama. Tunahitaji upinzani wenye nguvu ili kuweza kuleta mapinduzi katika Uchumi na maendeleo kwa ujumla.

Baraka
06-19-2009, 07:22 PM
Kwa kweli ni mtikisiko, lakini nadhani nitarudia kuongelea demokrasia. Neno hili kila mtu analiimba, lakini kwa tafsiri inayomridhisha. Kuondoka kwa Lwakatare ni pigo kubwa kwa CUF na wanahitaji kujipanga maana nadhani akiamua kuhama chama atahama na wafuasi wake, na balance ya upinzani itayumba, mizania itayumba kuelekea visiwani na bara kutapeperuka. Tunalaumu CCM, lakini ukiangalia vyama vyote vimejikuta katika tope lilelile. HAWATAKI KUACHIA MADARAKA, HAKUNA KUAMINIANA, WATU WANATAKA KUFA NA MADARAKA. UHAI WA CHAMA UNATEGEMEA FLEXIBILITY, INNOVATION NA INCLUSION. HIVI VYOTE VITAWEZEKANA KAMA TUNAAMINIANA. Bahati mbaya UMIMI umetawala, viongozi wengi wanajiona wao ni bora zaidi na mtu akileta changamoto ya maendeleo basi ni adui wa kushughulikiwa, YAMETOKEA CHADEMA, NCCR MAGEUZI, TLP NA CUF BILA KUSAHAU WAKONGWE CCM. ccm WANAAMINI KUWA NI WAO TU WA KUTAWALA, WAKATI KATIKA VYAMA, VIONGOZI WANAJIONA NI WAO TU WA KUONGOZA UPINZANI. Kwa kweli Lwakatare alikuwa anawakilisha kizazi kipya lakini akajikuta kanaswa na wavu wa viongozi wasiokubali changamoto