View Full Version : Huu ni uhuni wa kisiasa; ni wazimu wa kiuongozi!
mwanakijiji
06-19-2009, 08:45 AM
Jinsi Rais Kikwete alivyozungumzia jinsi uchumi wetu unavyokabiliwa na tishio la hali mbaya kufuatia msukosuko wa kiuchumi duniani, nisingetarajia kuona kwenye bajeti mipango au matumizi ya kijinga (na hapa namaanisha hivyo) kama ambayo tumeyasoma siku chache hizi.
Kwa vile niko kijijini sijapata nafasi ya kusoma threads zote na kwa kina gani haya yamejadiliwa. Kwamba, wanaokuja na kuomba omba fedha kwa ajili ya kunusuru uchumi wetu wanapanga kutumia karibu bilioni 60 kwa safari za viongozi na pia chai na vitumbua naweza kuelezea kwa maneno mawili tu; ni "uhuni" na ni "wazimu".
Ni uhuni, kwa sababu ni mtu mhuni ndiye ambaye anaweza akajaribu kufanya kitu ambacho anajua kabisa ni cha kijinga, cha kibabe na ambacho kitamnufaisha yeye zaidi kuliko mtu mwingine.
Ni wazimu, kwa sababu mtu mwenye akili timamu hawezi kwa upande mmoja kulia misaada, na upande mwingine kutumia utadhani fedha zinadondoka kama mvua!
Unrelated:
- Ka nzi kalioko Uswisi kamefuatilia kwa karibu safari ya jamaa yetu na mama yake na mkewe. Ila kanzi wamekabana sana, naona kanataka kurudi kijijini.
- Kumbe Al-Awadi ana mahusiano ya kindoa na kina Zayed; yule wa Loliondo? Well.. ndege wanaofanana, huruka pamoja. Sasa kwanini wasiseme tu kuwa ni "wale wale".. maana mwana wa mfalme alikuja tena juzi na maombi mengine. Nadhani JK atamridhia.
MM
Mponjoli
06-19-2009, 01:19 PM
Sasa mkuu, siku moja nilisoma comments za wasomaji kwenye Tanzania Daima, nikagundua watu wanakuchukia (wale waovu).. Mwandishi mmoja alitumia lugha ya kuudhi sana , inaelekea ndiyo sababu sasa Tanzania Daima hawana option ya online comment(what happened).
Lakini nafurahi kama wamegundua kwamba mwenye ze- utamu ni mtu wao, vinginevyio: Mh!.
Lakini zaidi naomba ufafanuzi: unadhani aliyepropose kodi kwa mashirika ya dini alikuwa na mtazamo finnyu?
Mie machache yananijia:
a) anaweza alikuwa amelenga wanasiasa fulani ambao huenda wakapata support kubwa ya kidini kwenye uchaguzi ujao
b) Hamtakii mema JK , hivyo akaona amfitinishe na mashirika hayo
c) Ni mbumbumbu ambaye hawezi kupima matokeo ya kitu anachofanya.
Vyovyote vile, Mkulo ameonyesha udhaifu mkubwa kwenye bajeti yake, na ndiyo maana Spika ameamua kutumia udikteta katika kumnusuru. Kuwaita watu kwa majina ili wapige kura ni uhuni wa wazi.
All in all, I can see a very tough election , next year. Tuendelee kuelimishana
mwanakijiji
06-19-2009, 09:37 PM
Hawa watu wanalipeleka taifa majaribuni, na siku hiyo ya mjaribu itakapofika watakuwa wa kwanza kushangaa "imefikaje". Wanajaribu sana uvumilivu wa watanzania. Lakini wanasahau kuwa hata punda ukimbebesha mizigo sana kuna siku hendi tena. Hugoma.
UF_alien
06-19-2009, 09:47 PM
Hakuna kinachonishangaza tena ktk nchi yetu........... Nitashangaa pale ukweli utakapoitwa ukweli na watu kuwajibika kwa yale wayafanyayo au wayasemayo.
Akajase
06-19-2009, 10:32 PM
Mkuu, umetumia neno uhuni na wendawazimu tu nafikiri mwalimu(Baba wa TAIFA la tanzania angelikuwapo leo, angetumia neno ushenzi. Si tukani, nataka kusema kitu hapa. Ikiwa aliweza kumwita mshenzi mtu yule aliyesema serikali yake kaiweka mfukoni si zaidi sana hawa wanaotaka kuyashibisha matumbo ya yao na kupanga mipango isiyo na tija? Twaweza tafakari badhi ya misamiati aliyoitumia akimanisha kupinga ubaguzia wa rangi, uhujumu uchumo na ukoloni mamboleo hata ile ya wkati wa vita dhidi ya Iddi amin Dada.
Ndiyo, wanastahili kuitwa washenzi kutokana na yale wanayoyafanya; mfano kutumia pesa ya bajeti ambayo bado kupitishwa. Wameona Bunge ni tambala la deni halina cha kufanya na waliomo humo ndani ni wendawazimu wenzao nothing to change.Shame! The great shame!
Ni bajeti ya waziri kihiyo[ si anacheti feki cha Master degree?] mwingi wa matkuwaita waandishi stupid; loh! Inakifu.
Ach-F
06-19-2009, 10:34 PM
Rais Kikwete hawezi kufanya lolote kwa walipa kodi wa Tanzania yeye ni Chukua Chako Mapema.
Pasco
06-20-2009, 08:41 AM
Samahi MMKJJ, mimi naomba kukoment kwenye ile unrelated ya kuhusu zeutamu, nawahakikishieni Tanzania haiwezi kufanya lolote kwa sababu mbili kuu,
1. Tanzania hatuna any Cyber Legistlation. Yaani hatuna sheria ihusuyo mambo ya
mtandao, hata akikamtwa atashitakiwa kwa sheria gani?.
2. Kama kosa limetendeka nje ya mipaka ya Tanzania, mahakama za Tanzania
hazina any jurisdiction za kusikiliza shauri lililofanyika nje ya Tanzania. Uthibitisho
wa hili mtaushudia hivi karibuni kwenye kesi ya Prof. Mahalu jinsi ule ushahidi wa
mtandao utakavyo pigwa chini kwa sababu sheria yetu ya ushahidi "Evidence Law"
haiutambui ushahidi wa aina hii.
Kitu ambacho serikali inaweza kufanya ni kumshitaki huko huko aliko, kosa la kweli
ni kama angeweka picha za watoto under "child pornography" lakini hizi za mtu
mzima, sijui.
kisa hiki cha zeutamu sasa ndio kitatufungua macho tuko nyuma kiasi gani, Sheria
ya Magazeti ya mwaka 1976 haiwezi lolote hapa ni kapa kapa kapa tupu.
Akajase
06-20-2009, 01:40 PM
Rais Kikwete hawezi kufanya lolote kwa walipa kodi wa Tanzania yeye ni Chukua Chako Mapema.
Hivi katika CCM na hata vyama vingine vya siasa hakuna mtu makini mwenye elimu na umri unaomruhusu kugombea kiti cha uraisi tukampa? Huyu jamaa ametuchosha. Ni mtu mwenye maono ya kuku, kufikiria leo na kesho itakuwaje hajui. Pengine nikisema kesho huenda nikawa nampendelea, niseme baadaye itakuwaje hajui.
Kwa miaka zaidi ya 10 alikuwa anautafuta urais, akaupata sasa miaka yote hiyo alikuwa na maono gani[kitugani cha kufanya kwa ajili ya Tanzania]; miaka 4 kathibitisha hakuna.
Mipango waliyopanga wenzake yeye ndiyo anatekeleza na mingine kuzidi kuharibu.Akheri ya J. Bokassa kuliko rais wangu wa sasa.
mwanakijiji
06-21-2009, 12:06 AM
Hilo la Utamu wala lisiwaumize kichwa; leo ndio nimetulia kidogo na kulifuatilia na habari ni kuwa jina ambalo limekuwa likitajwa kuhusika na mtandao huo hakuna ushahidi wowote kuwa mtu huyo anahusika na mtandao huo na watu wa serikali kwa kweli wanaonekana kuharibiwa mipango yao katika kufuatilia suala hili.
Nimefafanua zaidi kwenye hiyo mada yenyewe.
Powered by vBulletin™ Version 4.0.2 Copyright © 2012 vBulletin Solutions, Inc. All rights reserved.