PDA

View Full Version : Mmiliki wa ze utamu - Mtoto wa Kigogo wa CCM?



mwanakijiji
06-19-2009, 08:50 PM
Jina la mtoto wa mmoja wa wanasiasa wakongwe limekuwa likitajwa kuwa ndiye mmiliki au mhusika wa mtandao ambao umefungwa hivi sasa wa Ze Utamu. Kijana huyo ametajwa kuwa amejikuta kwenye matatizo baada ya mtandao anaodaiwa kuumiliki kurusha hewani picha ambazo zimetajwa kama zimemdhalilisha sana Rais wa nchi pamoja na viongozi wengine.

Vyanzo mbalimbali vinadokeza kuwa baada ya kugundulika kuwa mhusika ni mmoja wa vijana "wao" serikali imejikuta imepatwa na kigugumizi hasa baada ya baadhi ya watu waliowahi kukutwa na mtandao huo kujaribu kwa nguvu sana kuuhusisha mtandao huo ni wenu mtiifu. Lilikuwa tarajio lao wakubwa hao kwamba wangeweza kuua ndege wawili kwa jiwe moja lakini sasa inatafutwa jinsi ya kuweza kuzima kashfa hiyo kubwa.

Hata hivyo, kizuizi kingine ambacho kinaonekana ni cha kisheria zaidi kuwa huyo kijana inadaiwa ni raia wa Uingereza na kwa vile shughuli zake alikuwa anazifanyia uingereza basi ni givumu kumshtaki kwani kazi alizozifanya zinalindwa na uhuru wa kujieleza (freedom of expression).

Tunafuatilia suala hili kwa ukaribu!

Ach-F
06-19-2009, 09:27 PM
Kigugumizi wanachokipata kusema ni ndugu wa Malecela ni nini? Yeye aliona hilo ni jambo la maana kufanya na kama ana hatia kwa nini sheria isichukue mkondo wake? Haya ndio matatizo yale yale ya Ufisadi et al. Ukiamua kumgonga Nyani usimtazame usoni. Upuuzi huu tunauona kwa waliopewa dhana ya kulinda rasilimali ya taifa lakini wanapiga usingizi wa pono.

Hawatachukua hatua hadi wafahamu muhusika ni nani na anashirikiana nao kivipi katika kufilisi hazina ya walipa kodi.

Hilo la kusema yeye sio raia wa Tanzania ni upuuzi mtupu, huwezi kutegemea kutuletea hadithi za Abunuwasi hapa.

Pasco
06-20-2009, 07:46 AM
Kwenye hili la zeutamu, nawahakikishieni Tanzania haiwezi kufanya lolote kwa sababu mbili kuu,
1. Tanzania hatuna any Cyber Legistlation. Yaani hatuna sheria ihusuyo mambo ya
mtandao, hata akikamtwa atashitakiwa kwa sheria gani?.
2. Kama kosa limetendeka nje ya mipaka ya Tanzania, mahakama za Tanzania
hazina any jurisdiction za kusikiliza shauri lililofanyika nje ya Tanzania. Uthibitisho
wa hili mtaushudia hivi karibuni kwenye kesi ya Prof. Mahalu jinsi ule ushahidi wa
mtandao utakavyo pigwa chini kwa sababu sheria yetu ya ushahidi "Evidence Law"
haiutambui ushahidi wa aina hii.

Kitu ambacho serikali inaweza kufanya ni kumshitaki huko huko aliko, kosa la kweli
ni kama angeweka picha za watoto under "child pornography" lakini hizi za mtu
mzima, sijui.
kisa hiki cha zeutamu sasa ndio kitatufungua macho tuko nyuma kiasi gani, Sheria
ya Magazeti ya mwaka 1976 haiwezi lolote hapa ni kapa kapa kapa tupu.

Dua
06-20-2009, 12:19 PM
Wanashindwa kuwashughulikia mafisadi papa kama Rostum Aziz wataweza kushughulikia blogging? Wamalize kesi za Mramba na kikundi chake cha mafisadi waliokuwa wanaongozwa na Che-nkapa.

mwanakijiji
06-20-2009, 10:43 PM
Nimefuatilia kwa karibu jambo hili kwa ukaribu sana na habari ambazo zimevujishwa hadi hivi sasa kwa kiasi kikubwa zinadaiwa kuharibu uchunguzi na ya kuwa hazina msingi. Karibu vyanzo vyote vya kiusalama nyumbani (TISS na Polisi) ambavyo vyenye kujua juu ya hili vimeniambia pasipo shaka kuwa kutajwa kwa Male kwenye sakata hili hivi sasa kumeleta usumbufu usio wa lazima na hawaelewi ni kwanini ametajwa kama siyo kusudio la kujaribu kuvuruga uchunguzi.

Hata hivyo, vyanzo hivyo vimeshindwa kusema categorically kuwa anayehusika si mtoto wa kigogo yeyote na ni kwanini jina hilo limetajwa sehemu mbalimbali na kama kuna uhusiano wowote na mtandao wa zeutamu.

Maneno yao ni kuwa uchunguzi wao bado unaendelea na hakuna mtu aliyerudishwa Tanzania kwa sababu ya mtandao huo na kuwa masuala ya kisheria ni magumu zaidi kuliko inavyofikiriwa hasa kutokana na ukweli kuwa mmiliki na mwendeshaji wa mtandao huo yawezekana alikuwa/yuko nje ya nchi ambapo analindwa na sheria mbalimbali.

Uwezekano uliopo kwa mujibu wao ni kuwapata watu waliokuwa wanatuma taarifa za watu kutokea Tanzania ambao ndiyo itakuwa rahisi kuwashughulikia kisheria na jambo hilo siyo rahisi kulifanikisha mara moja kutokana na wingi wa malalamiko na madai.

Msimamo wangu kuhusu uchunguzi wa mtandao huu hauna shaka, ni upotezaji wa matumizi ya fedha za umma, muda wa watendaji na raslimali nyingine. Mnapotaka demokrasia muwe tayari kulipa gharama yake. Kama mnataka kuwa na kiwango fulani basi kipimo mnachotumia kitumike kwa wote wale wale. Haiwezekani akiandikwa Mwajuma mnakuwa kimya, akiandikwa James mnacheka lakini akiandikwa Mheshimiwa fulani basi mbingu zitikisike.

Katika haki za msingi (bill of rights) ambazo Katiba yetu inatambua hakuna haki "spesheli" za Rais au mbunge. Haki hizo za msingi ni za kila Mtanzania na ni lazima zilindwe hivyo. Mnapoamua kutozisimamia haki hizo kwa kwa Mwajuma na James (angalieni magazeti yenu ya udaku!) basi mnapoteza nguvu ya kimaadili ya kukemea pale mheshimiwa fulani anapoandikwa. Katiba inasema "kila mtu anastahili haki ya kutambuliwa na kuthaminiwa utu wake". Siku mkilielewa hili wazo la "kila mtu" basi mtajua kuwa cheo na hadhi ya kisiasa haimuongezei mtu mmoja "utu" zaidi au "heshima" zaidi au "thamani" zaidi".

Kati ya vitu ambavyo havinisumbui kichwa changu sasa hivi ni kuhusu mtandao wa zeutamu au mitandao mingine ya pornographia ambayo ipo kwenye internet! Vinginevyo, kuna watu wangekuwa hawalali, wengine wasingeenda kabisa makanisani, au mashuleni. Kwa kuliendeleza hili hata kujaribu kulifuatilia ni kupoteza muda na vipaji ambavyo vingeweza kutumika kwa mambo mengine mengi tu!
(Safarini Kijijini)

Daywell
07-09-2009, 11:34 AM
Kwanini tupoteze muda na mali ya watanzania kufuatilia kitu ambacho kwa mujibu wa walionitangulia sheria zetu hazina uwezo wa kumfanya chochote mmiliki wa ze utamu ni bora hizo rasilimali zikaelekezwa kwenye vipaumbele vingine! Na naamini mpaka hapa tulipofikia serikali itakuwa imejifunza na itaangalia uwezekano wa kuunda sheria zitazokidhi maisha haya ya sayansi na teke linalotujia kwa kasi ya ajabu!