PDA

View Full Version : Anatomy of Incompetence; A Pattern of Mediocrity



mwanakijiji
06-22-2009, 09:14 AM
1984- Masange JKT (Tabora) (Operesheni Nguvu Kazi) mlipuko wa baruti katika kutishia simba wala watu. Walijeruhiwa Luteni Usu Msange, Mwangupile (alikatwa mkono) na wengine kunusurika miongoni mwao mwandishi mashuhuri Chemi Che Mponda.

Januari 5, 1999 ? Bomu lalipuka pembeni ya Ofisi ya CCM, Kata ya Bulele, Muleba huko Kagera, jengo laharibiwa upande.

Disemba 25, 2005 ? Bomu laua 1, na watano wajeruhiwa kijiji cha Mlela Kigoma

Disemba 27, 2006 ? Bomu la mkono lalipuka Kurasini kwenye eneo la kukusanyia vyuma chakavu, mmoja afariki, 5 wajeruhiwa. Baada ya uchunguzi zaidi Mengine 43 yaligundilika kiwanda cha Quaim Steel Mills Chang?ombe, Dar na lingine moja lililookotwa ndani ya kiwanda cha Dabaga.

Mshangao mkubwa ni pale bomu mojawapo lilipokutwa linatumika kama mfuniko wa rejeta ya kijiko cha kupakia/kupakua mizigo ndani ya ghala la Hahrour Enterprises.

Oktoba 15, 2007 ? Bomu laua 4 wa familia moja huko Bukoba baada ya mtoto kuokota bomu hilo na kuliweka motoni akidhania kiazi. Mmoja ajeruhiwa.

Disemba 10, 2007 ? Watoto 3 wauawa na bomu Makutopora Dodoma, 6 wajeruhiwa

Mei 20, 2008 ? Kundi la Majambazi wapatao 15 wavamia basi walilipua kwa mabomu kwenye msitu wa Kimisi, Karagwe huko Kagera. 2 wauawa papo hapo. Mmoja ni askari mwenye silaha aliyekuwa akilisindikiza basi hilo. Aliuawa kishujaa lakini jina lake halikuimbwa kwa sifa kama alivyofanyiwa yule aliyeokoa mamilioni pale Ubungo!

Juni 9, 2008 - Helikopta ya Jeshi yaanguka na kulipuka, watu sita wafariki

Novemba 12, 2008, Mama na Mtoto wauawa na Bomu Kilosa wakiwa shambani.

Disemba 21, 2008 ? Watoto 4 wa jamii ya Kimasai walipuliwa na Bomu kijiji cha Embokoi, Siha huko Kilimanjaro karibu na bonde la Kilelepori ambapo Polisi hufanyia mazoezi ya silaha za moto

Januari 3, 2009 ? Bomu lalipuka Kambi ya Raha, mji wa Bomang?ombe huko Hai Kilimanjaro, 2 wajeruhiwa.

Feb 13, 2009 ? Washtakiwa 2 walipukiwa na Bomu Mahakamani Kasulu, Kigoma na mmoja kujeruhiwa katika jitihada za kutaka kutoroka.

Aprili 29, 2009- Mlipuko mkubwa wa mabomu ya kawaida na makombora watokea ghala ya silaha ya JWTZ kikosi cha 511 Mbagala ambapo watu 15 wauawa na zaidi ya 600 wajeruhiwa.

chokambaya
11-06-2009, 09:39 AM
Thou late,naomba iandikwe chronology ya sinema ya Richmond na PCB. Hivi tuna uongozi kweli nchini au tuko kwenye transition? From kuwa na serekali kuelekea kuwa kama Somalia?

Ach-F
11-06-2009, 08:08 PM
Unapoingia madarakani na kuona vinaelea lazima utambue ya kwamba waliokutangulia walikuwa wameweka misingi ambayo sio ya ki-Abunuwasi.

Serikali ya CCm inawaachia mafisadi wakubwa kuhujumu mali na rasilimali za taifa kama vile hazina mwenyewe. Wenyewe tupo na tutawatendea haki kwenye uchaguzi unaokuja.

Ni serikali gani hii ambayo imeshindwa kukusanya kodi ya kuwezesha watoto kwenda shule bila kuonewa kwa kukaa kwenye matofali?

Ni serikali gani hii ambayo imeshindwa kuona kwamba katika karne hii koroboi na vibatari hazitakiwi na tunahitaji umeme wa uhakika?

Ni serikali gani hii ambayo haioni umuhimu wa sera ya umwagiliaji kwenye mashamba na kuondokana na kutegemea mvua bila kuwa na upeo wa kukusanya maji?

Ni serikali gani hii ambayo haioni faida ya kutumia sarafu yake ambayo tumejichagulia na sio US dollars? Uzembe huu unafanya capital flight kuchukuliwa nje ya nchi bila kodi yoyote?

Ni Serikali gani hii ambayo inawafanya raia wake kuwa watumwa kwa wageni?

Ni serikali gani hii ambayo kila uchwao kunanuka milipuko ya Ufisadi? Je, kama ni hivyo tulipigania uhuru wa nini?