Steve Dii
06-25-2009, 10:26 PM
Kuna mtu aliniambia zamani kwamba Wahindi (wengi) hawawezi kukupatia chenji yako mtu mweusi (Mwafrika) baada ya kununua kitu dukani mwao kupitia mkono wao wa kulia. Niliambiwa sababu ni kwamba, wanaamini kufanya hivyo kwao ni kujitia mikosi katika biashara zao.
Nimeshaenda sehemu nyingi kwenye maduka yao, mara nyingi ni kweli kwamba kila nilipokutana na mhudumu wa Kihindi, chenji yako anakupatia kupitia mkono wa kushoto. Asipofanya hivyo basi anaiweka chenji juu ya meza kwenye counter.
Nilishawahi kukoromea wawili watatu hivi. But experience yangu inanipelekea kuamini kuwa hii labda ni kweli.
Nawaulizeni wana kijiji, je ni kweli hili jambo? Kuna mwenye habari zaidi kuhusiana na hili na vituko viendanavyo nalo?! Tuhabarishane.