mwanakijiji
06-30-2009, 06:38 AM
Kwamba Rais mstaafu Mkapa alitumia madaraka yake vibaya alipojipatia yeye na aliyekuwa Waziri wa Nishati na Madini Daniel Yona Mgodi wa Kiwira halina shaka. Kwamba katika kufanya hivyo alivunja Katiba na alipaswa kuondolewa madarakani kwa mujibu wa ibara ya 46 ya Katiba kwa kuvunja vipengele kadhaa vya sheria ya maadili ya viongozi wa umma ya 1995 na mabadiliko yake nalo halina shaka.
Chenye kuleta tatizo ni jaribio la serikali ya sasa kufanya makosa aliyoyafanya Mkapa akiwa madarakni kuwa ni kama "bahati mbaya" au "kupitiwa". Tatizo wanalolileta ni kuwa sheria haipaswi kufuatwa na watu wote na mtu ambaye ni Rais basi anaweza kufanya lolote atakalo akijua kuwa atatetewa.
Uamuzi wa kurudisha Kiwira mikononi mwa serikali ni ushahidi wa wazi kuwa Mkapa alifanya makosa ambayo kimsingi ukiunganisha na mambo mengine yalikuwa ni ya uvunjaji wa sheria na kwa hakika yangempasa afikishwe mahakamani kujibu mashtaka mazito dhidi yake.
Hata hivyo, Waziri Mkuu Pinda anasema mataifa ya nje yanamtambua na kumpenda Mkapa kwa kuwa ni mtu mwadilifu. Na zaidi ameliambia taifa kuwa anaamini kuwa Mkapa si "fisadi" kwa vile hana akaunti za dola nje ya nchi wala mandege yanayorushwa nchini.
Hivi ni nani alimuambia Mheshimiwa Pinda kuwa tatizo la ufisadi nchini ni watu kuwa na akaunti nje ya nchi? Kama hilo ni kweli anasema nini kuhusu Chenge ambaye ana akaunti ya mamilioni huko Uingereza na bado ni Mbunge?
Nimeandika kwa kirefu juu ya hili na ninatumaini itakuwa kwenye mojawapo ya magazeti ninayoandika siku ya Jumatano. Maswali ambayo natafuta majibu yake:
Ni kitu gani kitakufanya uridhike na kumsamehe Mkapa kwa kitendo chake? Je kurudisha Kiwira serikalini inatosha (kama vile aliyeiba ng'ombe akirudisha asishtakiwe kama wale wanaodaiwa kurudisha fedha za EPA?)
Je, sheria ifuate mkondo wake hata kama mhusika ni Rais mstaafu au tusiwaguse viongozi wetu wastaafu hata kama tunajua wamevunja sheria? Itakuwaje kama huko mbeleni tuje kusikie baadaye kuwa Rais fulani alipokuwa madarakani alimbaka mtumishi wake wa ndani, je tutamuachia kwa vile ni mstaafu?
NB: Ninafanya mambo kwa kibaba kutokana na hali ngumu ya uchumi kama mjuavyo japo kuna mambo mengi sana ya kufanya na kwa wale wanaojua mipango yetu KLHN kwa kweli sasa hivi tuko nyuma kwa karibu miezi mitatu. Tunaomba dua na sala zenu ili tuweze kufanikisha mipango yetu ili kuelekea 2010 mwamko mpya wa fikra uzidi kujikita miongoni mwa watu wetu.