View Full Version : BREAKING NEWS: CCM yashinda Biharamulo!
mwanakijiji
07-05-2009, 11:01 PM
Licha ya matokeo ya awali kuonesha CHADEMA kuongoza matokeo ya uchaguzi mdogo wa Biharamulo Magharibi, matokeo rasmi yanaonesha kuwa mgombea wa CCM ameibuka mshindi katika kinyang'anyiro hicho.
Ushindi huo umekuja wiki chache baada ya CCM kuibuka tena kidedea katika uchaguzi mdogo wa Jimbo la Busanda. Matumaini ya Chadema kuigaraza CCM yametupwa tena penbeni baada ya kazi hiyo kuonekana kuendelea kuwa ni ngumu zaidi kuliko inavyodhaniwa.
Hadi hivi sasa tunasubiri tamko rasmi la Chadema kufuatia kugeuka kwa upepo wa ushindi ambao ulionekana kuwafaa wao.
Nsaji Mpoki
07-06-2009, 10:47 AM
Taarifa nilizopata kutoka wa[pasha habari kutoka Biharamulo, ni kwamba hizo kura ni za waCCM wenyewe walikuwa hawamhitaji yule mgombea kwa sababu wanaona amepandikizwa.Wametumia njia nyingi kuzuia watu wengi waliojiandikisha wasione majina yao.Ndiyo maana unaona Makamba anahaha kwa sababu alijua waliopiga ni wanachama wake na idadi yao alikuwa nayo.Bahati mbaya hakujua kuwa wanachama wake hawakuwa na imani na mgombea Oscar Mukasa.Ikumbukwe baada ya kura ya maoni alimdhalilisha Mwenyekiti wa CCM-Biharamulo Anatoly Choya kuwa yeye ana tuhuma za rushwa hivyo angekuwa mzigo kwa CCM.Uropokaji wake huo uliwaudhi wafuasi wa Choya na wakaamua kupeleka kura zao CHADEMA.Alizungumza hivyo hadharani kama alivyofanya Tarime kwa kumdhalilisha Chambiri ambaye naye nitajiri na wafuasi kibao kuwa alikuwa hajaguliki matokeo yake akaangushwa na Marehemu Wangwe.Nafikiri hapa ndiyo kamba ya kumnyongea Makamba kwa kuropoka bila staha kwa wanachama wenziwe.
Dalali
07-06-2009, 01:01 PM
Mpoki,
Hii Haijaingii akilini kidogo.Inamaana kura zote zilizo CCM na CHADEMA ni zile zilizokuwa na PASS ya CCM na likely zilitakiwa kusema YES kwa CCM?
Hili zoezi la linafanyikaje katika macho ya waliokaribu na Biharamulo / Busanda .
Naomba ufafanuzi kidogo
mwanakijiji
07-06-2009, 10:27 PM
Tumebadili posting ya awali.
Ach-F
07-07-2009, 02:19 AM
Za mwizi arobaini. CCM waacheni waendelee, ... ... zikifika sijui watakimbilia wapi?
Nsaji Mpoki
07-09-2009, 12:29 PM
Mpoki,
Hii Haijaingii akilini kidogo.Inamaana kura zote zilizo CCM na CHADEMA ni zile zilizokuwa na PASS ya CCM na likely zilitakiwa kusema YES kwa CCM?
Hili zoezi la linafanyikaje katika macho ya waliokaribu na Biharamulo / Busanda .
Naomba ufafanuzi kidogo
Idara ya usalama wa Taifa kwa kushirikiana na Tume ya uchaguzi walianza kushughulikia mkakati wa kuisaidia CCM mara baada ya mahakama kuu kubatilisha ushindi wa Marehemu Kabuye.Ukumbuke vilevile kuwa CCM ina wajumbe wa nyumba kumikumi,ambao hutumika kuorodhesha watu wenye muelekeo wa kutoikubali CCM.Wajumbe hawa ni kiungo muhimu kati ya wapiga kura na CCM wilaya.Kutokea kwa wajumbe hawa CCM wilaya hukusanya majina hayo na kuyapeleka CCM makao makuu.
Sekretarieti ya makao makuu huwasiliana na IT unit ya NEC.Hapa ndipo wanaanza kuhamisha jina la mtu kutoka kituo alichojiandikisha na kupeleka kituo cha mbali na hivyo kumnyima nafasi ya kupiga kura.Matokeo yake mnaona turn-out inakuwa ndogo kila uchaguzi mdogo unapojitokeza.Njia ya pili ni kununua shahada ya watu wote wenye muelekeo ya kuikataa CCM na mauzauza yake hii mbinu ilitumika Tunduru.
Powered by vBulletin™ Version 4.0.2 Copyright © 2012 vBulletin Solutions, Inc. All rights reserved.