mwanakijiji
11-16-2008, 12:44 AM
Baada ya wabunge wa CCM kudai kuwa gazeti la Habari Leo (ambalo ni la serikali) liliandika habari ya Uchochezi Jumatano ya tarehe 5 Novemba, 2008 na kupendekeza hatua kali zichukuliwe, gazeti hilo limekuja na tahiriri ifutayo kuelezea sababu ya kuandika habari ile ambayo wengi waliifananisha na habari iliyoandikwa na gazeti la MwanaHalisi ambalo limefungiwa kwa tuhuma ya kuandika habari ya kichochezi.
Mhariri
Daily News; Saturday,November 08, 2008 @21:15
Moja ya sifa kubwa ya gazeti la HabariLeo ni uandishi makini unaozingatia misingi ya uandishi na uhariri wa habari. Ni sifa ambayo imeliwezesha gazeti hili kuwa chaguo la kwanza la wasomaji wenye kiu ya kupata habari na makala zilizoandikwa baada ya kufanyiwa utafiti wa kina. Wakati wote, HabariLeo linaongozwa na kanuni za uandishi wa habari.
Kwa umakini tulio nao, hatujawahi, na hatutathubutu, kutoa taarifa za kuokoteza au uzushi. HabariLeo, pamoja na gazeti mwenza la Daily News, ni vyanzo vya kuaminika vya habari. Ni magazeti rejea, sio tu kwa jina bali kwa sifa. Ni magazeti ambayo yana sera madhubuti. Habari zinazoandikwa na magazeti haya zinaongozwa na ukweli, hata kama ukweli huo unauma.
Na tunaamini tulichoandika kwenye taarifa yetu ya Novemba 5 ni ukweli. HabariLeo linaongozwa na dhima ya kuwatumikia Watanzania, kuiunga mkono serikali katika utekelezaji wa sera zake, na kuzieneza sera hizi. Gazeti hili ni nyenzo muhimu ya mawasiliano kati ya serikali na wananchi. Kutokana na umakini huo, na kutambulika kwa wajibu wa gazeti hili kwa jamii, wasomaji na wananchi kwa ujumla wanathamini habari na makala za gazeti hili.
Na hili bila shaka ndilo lililosababisha kutolewa, katika kikao cha mwisho cha Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania mjini Dodoma Ijumaa, kwa kauli za kushangaa habari iliyoandikwa katika gazeti la Jumatano tarehe 5 Novemba 2008 kuhusiana na mipango ya kundi dogo la wabunge wa Chama Cha Mapinduzi kutaka kumkosoa Mwenyekiti wao, ambaye ni Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, kuhusu namna alivyolishughulikia suala la malipo ya fedha za Akaunti ya Madeni ya Nje (EPA).
Kundi hilo, lilipanga kuwasilisha hoja kwenye mkutano wa ndani wa wabunge wa CCM uliopangwa kufanyika siku hiyo saa 10 jioni. HabariLeo lilipata taarifa za mpango huo kupitia vyanzo vyake vya kuaminika vya habari, na iliamua kuitoa taarifa bila kutaja majina ya wabunge kwenye kundi hilo, ingawaje tungeweza, kama tungetaka. Wakati utakapofika wa kuandaa orodha ya masuala ambayo Rais Jakaya Kikwete ameyashughulikia kwa kutumia kiwango cha juu cha busara, bila shaka suala la EPA litachukua nafasi yake muhimu.
Busara hizo zimeiwezesha nchi kurejesha Sh bilioni 70 ambazo tayari zimepangiwa kutumika kwa ajili ya mipango ya kuharakisha maendeleo ya taifa. Kwetu sisi, na kwa wote wanaochambua masuala kwa umakini ulionyooka, na kwa dhamira inayowakilisha nafsi ya ndani, tunapopata taarifa kwamba kuna mtu au kikundi cha watu kutaka kuanzisha mjadala usio na tija kwa nchi, na hasa mjadala huo unapolenga kumdhihaki Rais kwa kile alichokifanya kwa umakini, hatuwezi kukaa kimya.
Hili ndilo chimbuko la habari yetu kuu ya Jumatano Novemba 5. Wala asitokee mtu yeyote kuifananisha HabariLeo na gazeti lingine; kwani vyombo vya habari vinatekeleza majukumu katika misingi na dhamira tofauti. Kama walivyothibitisha hata wale ambao wamekosoa taarifa yetu, HabariLeo lina umakini ambao hauwezi kupuuzwa, wala kulinganishwa na gazeti lingine Tanzania, daima litasimama katika ukweli kutekeleza kazi zake kifanisi na kwa upeo wa hali ya juu ikitekeleza wajibu wake kwa umma na kwa taifa.
Wazo:
Sijaona sababu ya msingi kwanini gazeti hili lisichukuliwe hatua kama habari waliyoandika inalingana kabisa na habari iliyoandikwa na MwanaHalisi? Inaonekana sababu pekee ya kutochukuliwa hatua ni sababu ya kuwa gazeti la serikali.