PDA

View Full Version : Majambazi yavamia MNB Temeke kwa mabomu; mmoja auawa; mamilioni yaporwa

mwanakijiji
07-31-2009, 07:31 PM
Habari ambazo zinaendelea kutiririka zinasema kuwa ujambazi wa aina yake umetokea kwenye tawi la benki ya MNB huko Temeke jijini Dar ambapo watu wanaosadikiwa kuwa ni majambazi wamevamia benki hiyo na kupora mamilioni ya shilingi.

Uvamizi huo ambao unaonekana kuwa ni wa aina yake umefanywa kwa kutumia silaha kali na mabomu ya kurushwa kwa mkono ambapo mtu mmoja ameuawa na wengine kujeruhiwa. Msako mkali wa polisi unaendelea jijini Dar na maeneo ya jirani ili kuwatia mbaroni wale wote wanaohusika na tukio hili.

KLHN inatoa pole kwa familia ya marehemu na kuwaombea faraja wale wote waliodhurika katika kitendo hiki cha kihuni na cha uhalifu uliokubuhu. Picha kwa hisani ya Mroki.

http://www.mwanakijiji.com/images/stories/habari/gallery/tmk4.jpg

http://www.mwanakijiji.com/images/stories/habari/gallery/tmk5.jpg

http://www.mwanakijiji.com/images/stories/habari/gallery/tmk6.jpg

Ach-F
07-31-2009, 11:03 PM
Inasikitisha kuona matukio kama haya ambayo yalikuwa ni hadithi tu nchini Tanzania. Hii inatokana na utawala ambao unashindwa kusimamia haki kwa raia wake. Iweje majambazi yapore kiasi kikubwa namna hiyo? Sheria za benki pesa huwa zinakuwa kwenye usalama wa hali ya juu na ni kiasi kidogo tu huwa kinakuwa kwa makarani.

Ukishaanza kula nyama ya binadamu huwezi kuacha na madhara yake ndiyo haya. Je, Serikali inayoongozwa na mafisadi inaweza kweli kutoa ulinzi kwa raia wake?

Dua
08-01-2009, 04:37 PM
http://www.mwanakijiji.com/images/stories/habari/gallery/tmk5.jpg

Poleni wafiwa, lakini hapa ni lazima viongozi wanaosimamia usalama wa raia wawajibishwe. Yaliyotokea Ubungo yalikuwa hayatoshi? Ni lini tutajifunza kutokana na makosa ya nyuma?

Hivi polisi huwa wameshidwa nini kufanya analysis ya kuwaweka raia katika usalama, think of it magari watu wanatembea na silaha nzito kama hizi tena bila wasi wasi au tunasubiri msafara wa rais au waziri mkuu ushambuliwe ndio tuanze kuwa na system inayofanya kazi? Haya ni mambo ya aibu hata kuandika na sitegemei kama makamanda wa polisi wa Dar es Salaam bado wana kazi let alone the minister himself of Home affairs ambaye for a very long time tumesema hana uwezo pale alipo na ni aibu. A responsible person will resign without asking.

mwanakijiji
08-01-2009, 08:11 PM
Hadi hivi sasa hawajafanikiwa kuwapata... yaani watu 15 wanaweza kupotea kama mvuke namna hii..

son of alaska
08-01-2009, 09:39 PM
bongo imeshakuwa BAGHDAD,machine gun na magrenade waziwazi

mwanakijiji
08-01-2009, 11:44 PM
bongo imeshakuwa BAGHDAD,machine gun na magrenade waziwazi

wenyewe ukiwambia hivyo watasema unaitikia nchi yako mabaya!

mwanakijiji
08-04-2009, 08:20 PM
Imehaririwa: 04.08.2009 0101 EAT Gazeti: Uhuru

• UPORAJI NMB TEMEKE

sogeza Habari Nyingine
• Uporaji NMB Temeke: 03.08.2009 [Habari Zaidi]
• Hukumu ya Hakimu wa Temeke leo 22.05.2009 [Habari Zaidi]
• Sakata la maiti Temeke 06.11.2008 [Habari Zaidi]

Polisi D’Salaam yakamata sita

ITIKA KAGUBILA, TUDARCO NA KHADIJA MUSSA

JESHI la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, linawashikilia watu sita kwa tuhuma za kuhusika na tukio la ujambazi katika benki ya NMB tawi la Temeke, Dar es Salaam.

Aidha, polisi imetangaza kubadili mfumo wa ulinzi katika benki ikiwa ni hatua ya kuimarisha usalama sanjari na kuwabaini kwa haraka watu wanaoingia kwa lengo la kufanya uhalifu.

Hata hivyo, watuhumiwa hao hawakutajwa majina kwa madai kuwa hatua hiyo inaweza kuvuruga upelelezi na kwamba wanaendelea kuhojiwa kabla ya hatua kuchukuliwa.

Akizungumza na waandishi wa habari mjini Dar es Salaam, jana, Kamanda wa Polisi wa kanda hiyo, Kamishna Mwandamizi Msaidizi Suleiman Kova, alisema mbali ya kukamatwa kwa watuhumiwa hao, polisi wanaendelea na msako mkali kuhusu tukio hilo.

Kova alisema wameunda vitengo kwa ajili ya kuchunguza tukio hilo na namna lilivyofanyika ikiwa ni pamoja na kubaini silaha zilizotumika yakiwemo mabomu na mahali yalipotoka.

Alisema tangu kutokea kwa tukio hilo la uhalifu, polisi wamejipanga kuhakikisha wanapambana nao kwa kuwa inaonyesha watuhumiwa wana mbinu za kimataifa ambazo zinaweza kutishia usalama na amani ya nchi.

"Tunawashikilia watuhumiwa hawa na upelelezi wa kina unaendelea ili kuhakikisha tunawatia mbaroni wahusika wote. Huu ni uhalifu wa kimataifa na tuna wajibu wa kuudhibiti haraka iwezekanavyo kabla haujaleta madhara kwa nchi,” alisema Kova.

Kamanda Kova aliwasa wananchi kuwa makini na wageni wanaowapokea kutoka maeneo mbalimbali kwani kuna uwezekano wahalifu wa tukio hilo wametoka nchi jirani na waliwahi kushiriki kupigana vita.

Mwishoni mwa wiki iliyopita, majambazi yakiwa na silaha za kivita yakiwemo mabomu ya kutupwa kwa mkono, yalivamia benki ya NMB tawi la Temeke, Dar es Salaam na kupora zaidi ya sh. milioni 61.

Mbali na kufanya uporaji huo, majambazi hayo pia yalimuua mlinzi wa Kampuni ya Moku Security Services, Seif Mkwite, huku watu wengine 13 wakiwemo watumishi wa benki hiyo na wateja wakijeruhiwa.

Tayari polisi kupitia msemaji wake Abdallah Mssika, wametangaza donge nono la sh. milioni tano kwa mtu ama watu watakaotoa taarifa zitakazofanikisha kutiwa mbaroni kwa majambazi hayo.

Dua
08-05-2009, 12:38 AM
Imehaririwa: 04.08.2009 0101 EAT Gazeti: Uhuru

? UPORAJI NMB TEMEKE

sogeza Habari Nyingine
? Uporaji NMB Temeke: 03.08.2009 [Habari Zaidi]
? Hukumu ya Hakimu wa Temeke leo 22.05.2009 [Habari Zaidi]
? Sakata la maiti Temeke 06.11.2008 [Habari Zaidi]

Polisi D?Salaam yakamata sita

ITIKA KAGUBILA, TUDARCO NA KHADIJA MUSSA

JESHI la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, linawashikilia watu sita kwa tuhuma za kuhusika na tukio la ujambazi katika benki ya NMB tawi la Temeke, Dar es Salaam.

Aidha, polisi imetangaza kubadili mfumo wa ulinzi katika benki ikiwa ni hatua ya kuimarisha usalama sanjari na kuwabaini kwa haraka watu wanaoingia kwa lengo la kufanya uhalifu.

Hata hivyo, watuhumiwa hao hawakutajwa majina kwa madai kuwa hatua hiyo inaweza kuvuruga upelelezi na kwamba wanaendelea kuhojiwa kabla ya hatua kuchukuliwa.

Akizungumza na waandishi wa habari mjini Dar es Salaam, jana, Kamanda wa Polisi wa kanda hiyo, Kamishna Mwandamizi Msaidizi Suleiman Kova, alisema mbali ya kukamatwa kwa watuhumiwa hao, polisi wanaendelea na msako mkali kuhusu tukio hilo.

Kova alisema wameunda vitengo kwa ajili ya kuchunguza tukio hilo na namna lilivyofanyika ikiwa ni pamoja na kubaini silaha zilizotumika yakiwemo mabomu na mahali yalipotoka.

Alisema tangu kutokea kwa tukio hilo la uhalifu, polisi wamejipanga kuhakikisha wanapambana nao kwa kuwa inaonyesha watuhumiwa wana mbinu za kimataifa ambazo zinaweza kutishia usalama na amani ya nchi.

"Tunawashikilia watuhumiwa hawa na upelelezi wa kina unaendelea ili kuhakikisha tunawatia mbaroni wahusika wote. Huu ni uhalifu wa kimataifa na tuna wajibu wa kuudhibiti haraka iwezekanavyo kabla haujaleta madhara kwa nchi,? alisema Kova.

Kamanda Kova aliwasa wananchi kuwa makini na wageni wanaowapokea kutoka maeneo mbalimbali kwani kuna uwezekano wahalifu wa tukio hilo wametoka nchi jirani na waliwahi kushiriki kupigana vita.

Mwishoni mwa wiki iliyopita, majambazi yakiwa na silaha za kivita yakiwemo mabomu ya kutupwa kwa mkono, yalivamia benki ya NMB tawi la Temeke, Dar es Salaam na kupora zaidi ya sh. milioni 61.

Mbali na kufanya uporaji huo, majambazi hayo pia yalimuua mlinzi wa Kampuni ya Moku Security Services, Seif Mkwite, huku watu wengine 13 wakiwemo watumishi wa benki hiyo na wateja wakijeruhiwa.

Tayari polisi kupitia msemaji wake Abdallah Mssika, wametangaza donge nono la sh. milioni tano kwa mtu ama watu watakaotoa taarifa zitakazofanikisha kutiwa mbaroni kwa majambazi hayo .

Hivi hawa polisi wama akili timamu kweli? Unaweza kuita millioni tano donge nono? Maisha yamepotea halafu unakuja kutoa hako kamillioni tano kako na kuita donge nono? Hatuko serious. Absolutely ridiculous I can't get over this. ....

Max Shimba
08-05-2009, 05:32 PM
Inatia uchungu sana, hivi Rais kasema kitu hapa au kimyaaa

mwanakijiji
08-05-2009, 07:54 PM
Dua you are very right.. yaani mtu asnitch kwa shilingi milioni tano wakati uhai wa mtu umepotea? Donge nono lisingekuwa chini ya milioni 20. ndio maana wameshindwa kuzuia mauaji ya albino kwa sababu wanakuja na vidonge nono vya milioni 10!