mwanakijiji
08-01-2009, 07:15 PM
Imehaririwa: 01.08.2009 1107 EAT Gazeti: Uhuru
? Albino ajisalimisha polisi kuomba hifadhi
sogeza Habari Nyingine
? Albino auawa na kukatwa kiganja 25.09.2008 [Habari Zaidi]

? Mtoto albino auawa 19.02.2009 [Habari Zaidi]
NA MWANDISHI WETU, MWANZA
MLEMAVU wa ngozi Neema Ndalahwa, mkazi wa Mahina Ihago wilayani Nyamagana amejisalimisha Polisi kuomba hifadhi, baada ya kuwepo taarifa kuwa anasukiwa mipango ya kuuawa.
Neema (14) amejisalimisha katika Kituo Kikuu cha Polisi Julai 28, mwaka huu, ikiwa ni siku chache baada ya albino mwingine, mkazi wa Mahina kuuawa.
Wakati Neema akijisalimisha Polisi, albino wengine wameamua kuyakimbia makazi yao kwa hofu ya kuuawa ambapo, sasa wameomba kupewa ulinzi kwenye eneo waliloweka kambi.
Kamanda wa Polisi wa mkoa wa Mwanza, Jamal Rwambow, alisema, Neema aliomba hifadhi, baada ya kuzagaa kwa taarifa kuwa albino mwingine Dickson Kilingo, ameuawa wakati si kweli.
Kufuatia uvumi huo, Neema na mama yake mlezi Regina Fumbuka, waliingiwa na hofu ya kuuawa na hivyo kuamua kujisalimisha Polisi kuomba hifadhi.
Rwambow alisema Kilingo, ambaye ni msanii wa muziki wa kizazi kipya (Bongo flava), ameweka kambi kwenye hoteli ya Aspen mjini hapa, na kwamba mtu aliyevumisha taarifa hizo hana nia njema.
Kamanda huyo alieleza kwamba pamoja na uvumi huo, walimpokea kwa moyo mkunjufu binti huyo na kumpa hifadhi, ikiwa ni pamoja na malazi na chakula wakati wakisubiri Mkuu wa Wilaya ya Nyamagana, Cleophas Rugarabamu, kufanya utaratibu wa kumtafutia makazi.
Naye Mwenyekiti wa Chama cha Maalbino mkoani Mwanza, Alfred Kapole, ameliomba Jeshi la Polisi kuwapa ulinzi walemavu waliohama makazi yao kwa kuhofia kuuawa kwani, wimbi la mauaji linatisha.
My TAke:
Bunge hadi linaisha hakuna Mbunge wa CCM aliyepiga kelele kutaka Masha, Mwema, au RO kuwajibika; Hii ni aibu!