mwanakijiji
08-01-2009, 11:50 PM
Serikali yajipanga kuinusuru ATCL
na Habari zote na Hellen Ngoromera, Dodoma (Tanzania Daima)
SERIKALI imejipanga vema kuhakikisha Shirika la Ndege Tanzania (ATCL) ambalo utendaji kazi wake kwa sasa umekuwa wa kusuasua, linafufuka na kutoa huduma katika hali ya ushindani.
Kauli hiyo ilitolewa bungeni jana na Waziri Mkuu, Mizengo Pinda, alipokuwa akijibu maswali ya papo kwa papo.
Alilazimika kuweka hilo bayana wakati akijibu swali la Mbunge wa Busega, Raphael Chegeni (CCM), aliyetaka kujua hatima ya serikali kulifufua shirika hilo, pamoja na kutoa ahadi nyingi za kulinusuru.
Katika swali lake hilo, Chegeni alimuuliza waziri mkuu kwamba, serikali imekuwa ikitoa maamuzi mengi ambayo mwisho huwa haitekelezi, ikiwamo mwaka jana ambapo iliahidi kuifufua ATCL na hadi sasa hakuna kinachoendelea.
Akijibu swali hilo, Spika alisema serikali, inalipa kila aina ya nguvu shirika hilo ili lifanye kazi vizuri pamoja na matatizo ya fedha iliyonayo.
Pamoja na mambo mengine, Pinda alisema ATCL ina mambo mengi ambayo yanatakiwa kushughulikiwa na si kwa upande wa uongozi pekee, bali hata katika bodi yake na menejimenti kwa ujumla mambo ambayo serikali imejipanga kushughulikia.
My Take:
Hivi hawa watu waliachana lini kujipanga kuinusuru ATCL?