PDA

View Full Version : Mamiss watoto-Temeke!

Wakami
08-06-2009, 10:27 AM
:confused:
Wapendwa Watanzania,Jana kwenye taarifa ya habari ya Channel ten,taarifa za burudani na michezo,kuna eti sijui tamasha,sijui ni shindano la kutafuta miss Temeke kwa watoto wadogo miaka 6 hadi 11 hivi,hivi WATANZANIA labda mimi ndo sielewi watoto wetu tunawaandaaje jamani?

Kwa upeo wangu mdogo hayo mashindano hayafai kabisa na yangepigwa marufuku,badala ya watoto wafundishwe maarifa/taaluma mbalimbali sisi tunawaweka kambini eti wajifunze namna ya kutembea kama mamiss!Je wanasoma saa ngapi,wanapumzika saa ngapi!Na je hayo mashindano yanawasaidiaje hao watoto?

Kilichonikela sana jamani ehee eti mshindi wa kwanza atapata TV,na mshindi wa pili atapata redio,jamani WATANZANIA,ehee TV HUYO MTOTO WA MIAKA 6 inamsaidiaje?Zamani sijui siku hizi.ukifanya vizuri darasani,unapata zawadi ya MADAFTARI PAMOJA NA KALAMU ZA KUANDIKIA,Leo hii eti TV JAMANI!

Mbona hata wasitoe zawadi ya kumlipia ada ya masomo mpaka atakapomaliza chuo kikuu?Au hata wamnunulie sare ya shule?

WAANDAAJI HUO NI WIZI MTUPU,,MNAWATUMIA WATOTO KUTAKA KUJINUFAISHA NA HELA ZETU ZA VIINGILIO!

WADANGANYIKA TUSIPOKUWA MAKINI SHULE ZOTE ZITAFUTWA NA KUGEUZWA KAMBI ZA KUWAANDAA MAMISS!

SamGhaddaffi
08-06-2009, 02:27 PM
mawazo yako hayapishani sana na mawazo yangu mwanakijiji mwenzangu,tusipokuwa makini hii jamii ya wadanganyika tutakosa mwelekeo jaman,japokuwa tulionao unatia mashaka kama utatuelekeza kule tunakotaka..lkn hao jamaa si wamepewa kibali cha kuandaa hayo mashindano na hao mnaowaita serikali? nani wa kumfunga paka kengele

Wakami
08-06-2009, 04:24 PM
Asante Mwanakiji mwenzangu,inapobidi,,PANYA SASA AMFUNGE PAKA KENGELE!

mwanakijiji
08-06-2009, 05:23 PM
Wanakijiji wenzangu, naamini kabisa kuna vitabia vya ajabu sana ambavyo tumevianzisha na kuviendeleza na mojawapo ni hiki cha "Umiss somewhere". Tunafikia mahali tunawaangalia watoto wetu in terms of possible "u-miss" na badala ya kuangalia mtoto huyo kama daktari, mhandisi au mtaalamu wa baadaye.

Matokeo yake sasa tutafikia mahali tutaanzisha "u miss Utero"! Ni haya mawazo ya kutafuta fedha kwa namna yoyote ni lazima tujifunze kuweka mipaka.

Wamarekani na nchi nyingi za magharibi wamelipia vikubwa sana kwa hili la sexualization of babies!..

Ach-F
08-07-2009, 02:43 AM
:confused:
Wapendwa Watanzania,Jana kwenye taarifa ya habari ya Channel ten,taarifa za burudani na michezo,kuna eti sijui tamasha,sijui ni shindano la kutafuta miss Temeke kwa watoto wadogo miaka 6 hadi 11 hivi,hivi WATANZANIA labda mimi ndo sielewi watoto wetu tunawaandaaje jamani?

Kwa upeo wangu mdogo hayo mashindano hayafai kabisa na yangepigwa marufuku,badala ya watoto wafundishwe maarifa/taaluma mbalimbali sisi tunawaweka kambini eti wajifunze namna ya kutembea kama mamiss!Je wanasoma saa ngapi,wanapumzika saa ngapi!Na je hayo mashindano yanawasaidiaje hao watoto?

Kilichonikela sana jamani ehee eti mshindi wa kwanza atapata TV,na mshindi wa pili atapata redio,jamani WATANZANIA,ehee TV HUYO MTOTO WA MIAKA 6 inamsaidiaje?Zamani sijui siku hizi.ukifanya vizuri darasani,unapata zawadi ya MADAFTARI PAMOJA NA KALAMU ZA KUANDIKIA,Leo hii eti TV JAMANI!

Mbona hata wasitoe zawadi ya kumlipia ada ya masomo mpaka atakapomaliza chuo kikuu?Au hata wamnunulie sare ya shule?

WAANDAAJI HUO NI WIZI MTUPU,,MNAWATUMIA WATOTO KUTAKA KUJINUFAISHA NA HELA ZETU ZA VIINGILIO!

WADANGANYIKA TUSIPOKUWA MAKINI SHULE ZOTE ZITAFUTWA NA KUGEUZWA KAMBI ZA KUWAANDAA MAMISS!

Watanzania wameingia mjini kwa pupa. Hata nchi za ulaya ambazo ndio waanzishaji wa haya madudu huwezi kukuta waneweka kwenye prime time kwenye TV za dezo. Ujinga ni kitu kibaya sana.

mwanakijiji
08-07-2009, 05:33 PM
Wakati mwingine miye naona kana kwamba tunaiga tu alimradi na sisi tuonekane tunaiga.

Wakami
08-12-2009, 12:27 PM
Pamoja na kuiga kila linalokuja,nadhani hapa kikubwa sana ni kwamba WANAWATUMIA KUJINUFAHISHA!Wako kibiashara zaidi,ile dhana ya MTOTO WA MWENZIO NI WAKO ,UMLINDE,HAIPO!Sijui,lakini sijawahi kusikia kuwa mtoto wa Rundenga kawa miss Kinondoni au Kijitonyama mtaani kwake au hata ameshika nafasi ya kumi!Au hawa wenzetu,viongozi wa juu wa serikali kuanzia kwa mkuu wa kaya hii,kiranja mkuu,na viranja wadogo wadogo wao hawana watoto wa kike nao washiriki?,Hata wasipofanikiwa kutwaa taji,lakini tuwaone,jinsi wanavyofurahia kuwaona watoto wa wenzao ndani ya vivazi vya kulalia mbele ya kandamnasi tuone kama wanafurahia pia kuwaona watoto wao !

mwanakijiji
08-12-2009, 08:54 PM
Labda ndiyo fasheni yenyewe; hivi mara ya mwisho mtu kuandaa Spelling Bee Tanzania ilikuwa lini?