PDA

View Full Version : Huu ujambazi tena!!!



mwanakijiji
08-07-2009, 05:43 PM
7th August 2009
B-pepe
Chapa
Maoni

Watu wanaosadikiwa kuwa majambazi, wamevamia jengo la Taasisi ya Elimu (TIE) na kupora kompyuta 70 na magari mawili.

Kabla ya kufanya uporaji huo usiku wa kuamkia jana, waliwateka walinzi, wakawafunga kamba na kuwafungia ndani ya vyumba vya ofisi hizo, kisha wakafanya uhalifu huo.

Akizungumza huku machozi yakimtoka, Mkurugenzi wa TIE, Dk. Paul Mushi, alisema dalili zinaonyesha kuwa wizi huo ni hujuma kwani unalenga kufanya asasi hiyo ishindwe kutimiza wajibu wake kwa kuchukua vitendea kazi.

Moja ya magari yaliyoibwa lilikuwa aina ya benzi, mali ya Mkurugenzi huyo.

Nipashe ilipofika kwenye eneo la tukio jana asubuhi, iliwakuta askari polisi waliovaa kiraia wakiwafungua kamba walinzi wawili wa kampuni ya ulinzi ya Gema, ambao ndio waliokuwa wakilinda Jengo hilo.

Mlinzi mmoja wa jengo hilo aliyejitambulisha kwa jina la David Shauri, alisema majambazi hao walifika katika ofisi hizo saa 8:00 usiku na kuruka uzio, kisha kuwateka na kuwafunga kamba.

Alisema baada ya kuwafunga kamba yeye na mwenzake, waliingia kwenye chumba cha kuhifadhi funguo za ofisi na kuzichukua.

"Walitupiga sana na kutufunga mikono, wakachukua funguo na kutuleta ndani... mimi nikafungiwa humu (akionyesha chumba namba tatu), mwenzagu alifungiwa namba mbili...baada ya hapo, sikujua kilichoendelea," alisema.

Mlinzi mwingine, Winfrida Kaiwanga (33), mkazi wa Kimara jijini Dar es Salaam, alisema aliwasikia majambazi hao wakisema wametokea Temeke.

"Niliwasikia wakidai kuwa wametoka Temeke... lakini sikuwatambua maana waliniziba macho na kuniingizia vitambaa mdomoni," alisema.

Hata hivyo, hakuendelea kuzungumza baada ya kuamriwa apelekwe hospitalini kwa ajili ya kupatiwa matibabu kwa vile alionekana kuwa na hali mbaya.

CHANZO: NIPASHE

Ach-F
08-08-2009, 12:43 AM
Huo ndio tunaita ujinga. Hadi mashine 70 zinaibiwa .. Je, walikuwa na insurance? Kama walikuwa hawana Why? Machine hizo zilikuwa na security ya aina gani pale zilipo i.e. kama zilikuwa secured etc. Je walikuwa na alarms za aina yoyote?

Tanzania iko karne ya 19 wakati nchi nyingine ziko karne ya 21, where are you? workup!