PDA

View Full Version : Walimu wasisitiza kugoma



Mpita Njia
11-16-2008, 06:00 PM
Nimezungumza na Mwenyekiti wa Chama cha walimu, Bwana Gratian Mukoba leo anasema kuwa mgomo wao wa kesho upo palepale licha ya ahadi na vitisho vinavyotolewa na serikali. tena anasema kuwa ahadi na vitisho hivyo ni uthibitisho kuwa madai yao ni ya kweli.
Anachosema Mukoba:
Kwamba serikali imekwenda mahakamani kutaka mgomo huo uzuiwe haiitishi CWT kwa sababu hadi hivi sasa chama hicho hakijapokea summuns kutoka mahakama yoyote.
Tishio kuwa walimu watakaogoma watakatwa mishahara haliwatishi.
Ahadi kwamba fedha zimeanza kupelekwa wilayani haliwahusu, wanachotaka wao si fedha kupelekwa wilayani, bali walipwe madai yao.

Ach-F
11-21-2008, 12:59 AM
Pesa aliyotumia Jakaya Kikwete kuvinjari na kununua vipodozi ugenini ingewatosha walimu.

dRU
01-05-2009, 03:27 PM
Pesa aliyotumia Jakaya Kikwete kuvinjari na kununua vipodozi ugenini ingewatosha walimu.
Kuna mambo ambayo yanahitaji uelewa na yumkini kuuliza kwa kupata kujua jambo. Hakika uongozi ni jalala ambapo kila taka itatupwa hapo. Hili swala la mishahara ya waalimu si la kumlaumu Rais Kikwete hili ni swala la watendaji wa tena ngazi za chini kabisa za utekelezaji wa maswala kama haya ya malipo. Na yote hii inaletwa na ile "u-mimi", "u-kwanini" basi ilimradi pawepo na kasababu ama ka mwanya ka kupata kitu kidogo. Leo hii kama nchi hii tungekupa wewe basi labda yangekuwa matokea mabaya zaidi ya haya ama mazuri lakini jambo muhimu kuelewa ni kwamba UTAWALA ndani ya UTAWALA si sawa na UTAWALA nje ya UTAWALA.. utaona mapungufu mengi ukiwa nje na ukiwa ndani utaona Ugumu wa kuyatatua mapungufu hayo ulivyo... waswahili wanasema "Achekaye kovu hajaona jeraha".:D:D