PDA

View Full Version : CCM kuna ufisadi - Askofu Kilaini



mwanakijiji
08-12-2009, 08:39 PM
Ufisadi CCM upo- Kilaini (Majira)
Wednesday, 12 August 2009 07:02
*Asema dawa si kujifariji ni kuwang'oa wote wanaohusika
*Amtaka Mahanga aoneshe mfano kwa kutaja wale anaowajua
*Lipumba naye agonga msumari,asema uovu huo uko wazi

Na Edmund Mihale

ASKOFU Mkuu Msaidizi wa Kanisa Katoliki Jimbo Kuu la Dar es Salaam, Muhashamu Dkt. Methodius Kilaini amesema ufisadi ndani Chama Cha Mpinduzi (CCM) upo na haufichiki na dawa yake ni kuwang'oa wanaohusika ndani chama hicho.


Kauli hiyo ya Askofu Kilaini imekuja siku moja baada ya Naibu Waziri wa kazi Ajira na Maendeleo ya Vijana, Dkt. Makongoro Mahanga kuwataka wanachama wa hicho kuacha kutoa tuhuma za ufisadi kwa wenzao bila kufuata taratibu kwa madai kwamba kufanya hivyo ni kukiharibia chama hicho.

Katika taarifa yake kwa vyombo vya habari Dkt. Makongoro Mahanga alieleza kuwa wapinzani kushutumu CCM ni mbinu kawaida katika medani za kisiasa na tuhuma nyingi za ufisadi zinazokiandamana chama hicho ni zakufikirika kwani hazina ushahidi wa kutosha.

Aliwataka wanaCCM wenzake kutumia vikao vya chama kumaliza matatizo yao ili kuepuka kuwapa faida maadui wa chama kwa shutuma za namna hiyo.

Akizungumza na Majira jana kwa njia ya simu Askofu Kilaini, alisema hata kama CCM itatumia vikao vya chama kumaliza tatizo la ufisadi lakini dawa pekee ni kuwatimua wote wanaotuhumiwa ili kujenga imani ya chama hicho kwa wananchi.


"Mimi najua ufisadi upo ndani ya chama hicho na dawa ya kuuondoa ni kuwafukuza wote wanaotuhumiwa iwe kwa kutumia vikao husika au vyombo vya sheria," alishauri Askofu Kilaini


Alisema siku hizi neno ufisadi limekuwa wimbo unaoimbwa na kila mtu hata yule anayetuhumiwa kuwa fisadi na kupoteza maana yake.

Ameishauri CCM kuhakikisha inawachulia hatua kali wanachama wote wanaohusishwa na tuhuma za ufisadi ili kukinusuru chama hicho.


Alisema kwa kuwa Dkt. Mahanga amekiri kuwa kuna watu wachache ambao si waadilifu ndani ya chama hicho wanaokabiliwa na tuhuma za ufisadi, hivyo ni bora aoneshe mfano kwa kuwataja kwani kwa kufanya hivyo atakuwa amekiokoa chama hicho.

"Nia ya Dkt. Mahanga kukilinda chama ni nzuri lakini si kwa kuwaficha wanaotuhumiwa kwa ufisadi, dawa ni kufanya vikao na kufichua sambamba na kuwafukuza katika chama hicho," alisema Askofu Kilaini.

Naye Mwenyekiti wa Chama cha wananchi (CUF) Profesa Ibrahim Lipumba amesema tuhuma za ufisadi zinazowakabili viongozi na makada wa Chama cha Mapinduzi ziko wazi na haziwezi kuepukika kwani zina ushahidi wa kutosha.

Prof. Lipumba, alisema kauli ya Dkt. Mahanga ni yakujikosha kwani ufisadi ndani ya CCM si jambo la kuficha na liko wazi kwa kila mtu.


Alidai kuwa katika sakata la fedha za Akaunti ya Madeni ya Nje (EPA) zilizochotwa kutoka Benki Kuu ya Tanzania (BoT) na baadhi ya watuhumiwa kufikishwa mbele ya vyombo vya sheria, kampuni ya Kagoda ambayo ni moja ya zinazotuhumiwa kwa ufisadi huo imehusishwa na baadhi ya makada wa CCM.

My Take:
Je ndio wakati umefika ambapo mgongano kati ya Kanisa na CCM unazidi kuiva hasa baada ya ule "waraka" wao? Je viongozi wa dini nyingine nao wanaweza kuita shoka shoka na jembe ni jembe?