PDA

View Full Version : Wamiliki wa mabasi waanze kuwajibishwa ikitokea ajali?

mwanakijiji
08-14-2009, 05:39 PM
Kwa muda mrefu tumekuwa tukiwatupia lawama madereva wa mabasi inapotokea ajali na kama tishio la mgomo wa leo linavyoonesha kwa kufanya hivyo tumewafumbia macho wamiliki wa mabasi hayo ambao ndio wenye jukumu la kuajiri madereva wazuri, kuwa na magari yaliyo katika hali nzuri na kutoa mafunzo ya refresher kwa madereva.

Ach-F
08-17-2009, 05:49 PM

Tatizo sio madereva wala wenye mabasi, ni serikali ya CCM ambayo haifuati kanuni na taratibu za sheria ambapo wameweza kabisa kuhalalisha ukiritimba katika kila nyanja.

Sheria za usalama barabarani zipo wazi na hakuna sababu yoyote ya serikali kupoteza muda wa askari wa usalama kwenda barabarani na kuona sheria zinafuatwa. Technologia hivi sasa ipo na ni rahisi kabisa kuweka Cameras kwenye sehemu mbali mbali (Strategically) na kuweza kuwashika wale wote wanaokiuka sheria za usalama Barabarani kwa faini ambapo hakuna ulalamishi - wewe ni kukusanya pesa tu ambayo itaongeza vitendea kazi na kufanya Jeshi la polisi kuwa imara zaidi. Mifano ipo mingi sisi tupo katika ice age kila tunachofanya ni cha old age. Wake up Tanzanians and use technology.