mwanakijiji
08-17-2009, 09:13 PM
Hatimaye kesi ya mauaji iliyokuwa ikimkabili aliyekuwa Mkuu wa Upelelezi jijini Dar Bw. Abdallah Zombe imefikia tamati katika mahakama kuu baada ya Mahakama hiyo kumuona hana hatia yeye na wenzake. Kesi hiyo iliyodumu kwa karibu miaka mitatu sasa imehitimiza giza kubwa lililotanda juu ya Bw. Zombe na maafisa wenzake wa Polisi ambao walikuwa wakituhumiwa kuwaua wafanyabiashara wanne wakidhania kuwa ni majambazi.
http://www.mwanakijiji.com/images/stories/habari/people/zombe.jpg
Je haki imetendeka?
Ach-F
08-18-2009, 12:57 AM
Tunasubiri kuachiliwa kwa Mramba et al.
Wakami
08-18-2009, 11:59 AM
Mimi nina wazo binafsi,Hii kesi ya Zombe na wenzake imechukua muda mrefu sana,hela nyingi sana za walalahoi walipa kodi Wadanganyika zimepotea sana,naamini zingetosha kuwalipia wasomi wetu vyuo vikuu hata kwa miaka 2 wote!Sasa kama hayo ndio tunayoyategemea kwenye zile kesi za akina Mramba et al,si ni bora kesi zao nao ziishe kesho Jtano,ushahidi wa kuwatia hatiani haupo/hauko wazi hivyo mimi kama Chaji Sumata kwa mamlaka niliyopewa na mheshimiwa J,na kwa mujibu wa sheria za enji hii,nawaachia huru,Wadanganyika ambao hamkuridhishwa na hukumu hii,mna uhuru wa kukata rufaa,KOOOOTI!Mranba waziri wa fedha na Lowasa waziri mkuu,mwakani mwezi wa kumi,si hawana makosa jamani?
Wadanganyika TUSIDANGANYIKE,hizo kesi nazo bora ziishe na wote waachiwe huru,hele za kushughulika kesi zifanye mambo mengine,hata ziwe za kampeni uchaguzi ujao mwakani.
Ila ukweli utabaki uleule,MUNGU SI ATHUMANI,Msalimieni sana DITOPILE!Mwabieni tumemkumbuka!
Powered by vBulletin™ Version 4.0.2 Copyright © 2012 vBulletin Solutions, Inc. All rights reserved.