PDA

View Full Version : Je CCM watatumia EO style mwaka 2010??



Ng'wana Diyu
08-21-2009, 05:27 PM
Baada ya kusoma report ya Meremeta sasa nimejua kwa nini mashirika mengi ya Umma yaliuzwa kwa raia wa Afrika Kusini (Makaburu), Makaburu waliujua udhaifu wa nchi nying wakati wa vita ya Ubaguzi. Na baada ya kuona wasingeweza kuendelea kuitawala SA kwa njia ile wakabuni namna ya kututawala (siyo tu SA bali hata zile nchi zilizokuwa huru kama Tanzania), na ukiangalia mbinu zinazotumiwa na vyama tawala katika mataifa mengi ya Africa (Tanzania, Kenya, Uganda, n.k) ni mbinu za kijasusi na wanafanya kila linalowezekana angalau kutangaza matokeo wanayoyataka hata kama mazingira yote yanaonyesha kushindwa. Mifano ni mingi... nitaitaja michache. 2005 Ubungo - Mnyika alionekana atashinda kwa kishindo dhidi ya Kaenja (matokeo wote tunayajua), Busanda na Biharamuro vivyo hivyo (sasa wameamua sasa kuanzisha jeshi lao kwa ajili ya kuwatishia wote wanaotaka kuona kura haziibwi, wanawapiga na kuwatishia.
Mwaka 2010 unaweza ukawa mwaka mhimu sana katika historia ya Tanzania. Kwanza tuwashukuru sana wote waliofanikisha report ya Meremeta, inaweza kuwa kazi moja ambayo inaweza kuleta madiriko Tanzania kwan angalau sasa tunajua kinachofanyika nyuma ya mapazia na mda uliobaki unaweza ukawabana kamati yao ya ufundi ya namna ya kuiba kwani mbinu na vikundi vyao vya maangamizi vinawekwa hadharani.
Tuwaoombee wabunge wote wa CCM wawe wajasiri vya kutosha wakiona hawawezi kusema kwa uwazi na uhuru wakiache chama chao waungane nasi katika mapambano... ila Mamuluki wote tuwaombee kwa Mungu washindwe na walegee wasije wakavimaliza vyama vilivyopo kama walivyokiua NCCR na TLP.
Mungu ibariki Tanzania. Amen

mwanakijiji
08-22-2009, 08:35 PM
Mambo yote haya yan mwisho kwa kweli. Hakuna kitu ambacho wanaweza kufanya ambacho kitaiokoa CCM kutoka huko iliko.