PDA

View Full Version : Cheyo naye!



mwanakijiji
08-22-2009, 09:38 PM
Cheyo: Naiombea CCM isambaratike kwa amani


na Sammy Lothy, Shinyanga




MWENYEKITI wa UDP , John Cheyo ameomba dua ya kukiombea Chama Cha Mapinduzi (CCM) kisisambaratike vibaya bali kwa amani licha ya kuwa kusambaratika kwa CCM ni fahari kubwa kwa kambi ya upinzani nchini.

Cheyo, alitoa kauli hiyo jana alipozungmza na Tanzania Daima juu ya hali ya kisiasa nchini na maendeleo ya Jimbo lake la Bariadi Mashariki.

Alisema kuna dalili kubwa ndani ya chama hicho tawala kusambaratika kwa kile alichodai kuwa kumekuwa na malumbano miongoni mwa viongozi, jambo ambalo limetishia baadhi ya viongozi wa juu kufukuzwa uanachama.

?Angalia CCM wanavyokwenda, huyu anakwenda hivi yule akwenda hivi, wakisambaratika vibaya nchi itakwenda pabaya, amani itakuwa mashakani, jambo ambalo limetishia baadhi ya viongozi ndani ya chama hicho kutishiwa kuvuliwa uanachama,? alisema.

Alisema ili CCM isisambaratike vibaya haina budi kupambana kufa na kupona na ufisadi kwa kuliondoa kundi hilo ndani ya CCM na kuwa wale ambao wanashindwa kuvumilia ni busara sasa wakajiunga katika kambi ya upinzani.

Mwenyekiti huyo alimbeza Katibu Mkuu wa CCM, Yusuph Makamba, jinsi anavyoviponda vyama vya upinzani na badala yake amemtaka ajipange kikamilifu kuliondoa kundi la ufisadi ndani ya chama chake.

Kundi jingine ambalo amemshauri Makamba hana budi kulishughulikia na CCM yenyewe ni la wanasiasa wasio na msimamo ndani ya chama hicho na wale wenye fedha ambao wamekuwa wakikitumia chama kwa manufaa yao binafsi.

Eneo jingine alilolisema ni lile la utawala na uongozi bora wa sheria na haki ambao wamekuwa wakiyatumia vibaya madaraka na nafasi walizonazo na kutomsaidia Rais Jakaya Kikwete.

Kuhusu maendeleo ya wilaya yake, mbunge huyo alisema kuna mafanikio makubwa katika nyaja za elimu, miundombinu na kuwa mafanikio hayo yote yametokana na kazi nzuri ya Rais Kikwete.