PDA

View Full Version : Gazeti laamriwa kumlipa Mengi Bilioni1.5)



mwanakijiji
08-25-2009, 06:29 AM
Gazeti latakiwa kumlipa Mengi bil. 1.5/-


na Ratifa Baranyikwa (Tanzania Daima)



MAHAKAMA Kuu Kanda ya Dar es Salaam, imemwamuru Mhariri wa Gazeti la Changamoto, Erick Antony pamoja na Kampuni inayochapisha gazeti hilo, Ladyband Company Limited kumlipa Mwenyekiti wa Makampuni ya IPP, Reginald Mengi fidia ya sh bilioni 1.5 kwa kuandika habari za uongo dhidi yake.

Hukumu hiyo ilitolewa jana na Jaji Geofrey Shaidi wa mahakama hiyo kutokana na kesi ya madai namba 35 ya mwaka 2009, iliyofunguliwa Machi 11, mwaka huu na Mengi aliyekuwa akiwakilishwa na wakili Michael Ngalo dhidi ya mhariri na kampuni inayochapisha gazeti hilo.

Katika hati yake ya madai, Mengi alikuwa akilalamikia habari mbili zilizochapishwa na kusambazwa na gazeti hilo katika matoleo yake namba 132 na 135, moja ikiwa na kichwa cha habari ?Mengi kuitia hasara serikali?.

Habari nyingine ni ?Uchaguzi Mdogo Mbeya Vijijini? ambayo ilikuwa imebeba vichwa vya habari vingine vidogo; ?CHADEMA yaanika silaha?, ?Mengi kuombwa kuchangia, kuendesha kupaa na helikopta?.

Katika hukumu hiyo, mahakama hiyo ilisema kuwa baada ya kutathimini madai ya ushahidi wa Mengi na vipengele kadhaa vya sheria kuhusu kesi za kashfa, mahakama iliridhika kuwa Mengi amethibitisha kesi na madai dhidi ya wadaiwa kwa kiwango kinachotakiwa kisheria.

Mbali na mhariri pamoja na kampuni hiyo kutakiwa kumlipa mwenyekiti huyo kiasi hicho cha fedha, pia wametakiwa wafute machapisho yote yaliyolalamikiwa na Mengi.

Mahakama pia imetoa amri kwa gazeti hilo kumuomba radhi Mengi, na wachapishe ufutwaji huo na radhi mara tatu mfululizo katika gazeti la Changamoto.

Mahakama pia imelitaka gazeti hilo kutorudia kuandika, kutoa, kusambaza habari zilizolalamikiwa au yoyote inayomuhusu Mengi kabla ya kuwasiliana nae.

Mbali na hayo, pia wametakiwa walipe riba kwenye hizo fidia kwa kiwango cha asilimia 12 toka siku ya hukumu hadi siku ya mwisho wa malipo na wamlipe Mengi gharama zote alizoingia katika shauri hilo na riba ya asilimia 12 toka siku ya hukumu hadi siku ya mwisho ya kulipa.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa kwenye vyombo vya habari kuhusu hukumu hiyo, habari iliyoandikwa na gazeti hilo; ?Mengi kuitia serikali hasara?, ilieleza kuwa, serikali huenda ikajikuta inapoteza sh bilioni 28 ikiwa ni pamoja na riba iwapo haitakata rufaa dhidi ya Benki Kuu ya Tanzania na wenzake.

Habari hiyo imedaiwa na mahakama kuwa ilipotosha kwa makusudi ukweli wa maamuzi ya Mahakama Kuu ya Tanzania katika kesi ya madai namba 197/193 yaliyotolewa Septemba 30, 2008.

Aidha, hukumu hiyo imekuja baada ya washitakiwa ambao ni Erick pamoja na kampuni inayochapisha gazeti hilo, kutowasilisha utetezi pamoja na kuhudhuria mahakamani.

Kutokana na hilo, mahakama imedai imewaona wadaiwa kuwa wameidharau na kutoa onyo dhidi yao.

Dua
08-25-2009, 08:40 PM
Nani anamiliki hilo gazeti? Je, wataweza kulipa? Je, hicho kiwango ni proportionate na uchafuzi uliofanywa?