Wanavyojua kutumia fedha zetu! hawana hata uchungu!
Ukumbi wa Bunge kubomolewa
na Mwandishi wetu, Dodoma
UKUMBI mpya wa Bunge la Jamhuri ya Muungano, unaotumika kwa shughuli za Bunge utavunjwa na kusukwa upya ili kuruhusu utengenezaji wa viti vya kisasa vitakavyofungwa vifaa maalumu vya mawasiliano ya teknolojia ya kisasa.
Hatua hiyo pia itaongeza idadi ya viti kutoka 340 vya sasa hadi viti 360 ili kumudu idadi ya wabunge wanaotarajiwa kuongezeka katika Bunge lijalo.
Itakumbukwa jengo hilo ambalo ni la kwanza Afrika Mashariki na la tatu kwa Bara la Afrika, hadi kukamilika kwake liligharimu zaidi ya sh bilioni 30.9.
Hatua hiyo ilitangazwa jana na Spika wa Bunge, Samuel Sitta, wakati akitoa mwongozo wa kiti cha Spika, kutokana na hoja iliyoibuliwa na Mbunge wa Ukerewe, Gertrude Mongela, aliyehoji sababu za Bunge kutumia teknolojia ya zamani kuhesabu kura za ndiyo na hapana zilizopigwa kwa wabunge ili kuunga mkono au kupinga hotuba ya Bajeti ya Serikali ya mwaka 2010/2011.
Akifafanua muundo mpya wa Bunge, Spika Sitta alisema kila kiti cha mbunge kitakuwa na runinga pamoja na mawasilino ya kisasa ya kompyuta, ambayo yatamwezesha kuuliza swali na kupata majibu kutoka kwa waziri anayehusika bila kusimama wala kutumia vikaratasi.
“Kwanini tunatumia teknolojia ya zamani, jibu lake ni dogo tu, ni kwamba hili jengo viti vyake vitafumuliwa vyote na kusukwa upya na kazi hiyo itafanyika mara baada ya kuvujwa Bunge. Michoro ya kazi hiyo imeshakamilika na kazi hiyo imefanywa na Mbunge wa Hai, Fuya Kimbita (CCM), yeye na ujumbe wake wamekwenda kwenye mabunge ya Scotland na mabunge mengine kuangalia jinsi ya kulirekebisha Bunge letu liwe la kisasa zaidi,” alisema Spika Sitta.
Katika hatua nyingine, Waziri Mkuu Mizengo Pinda amekitetea Chama Cha Mapinduzi (CCM) bungeni kuhusu utekelezaji wa Ilani yake ya uchaguzi kuwa bado unaendelea katika mwaka wa fedha 2010/2011.
Akijibu swali la nyongeza la Mbunge wa Viti Maalumu, Susan Lyimo (CHADEMA), aliyehoji kutotekelezwa kikamilifu kwa ilani ya Chama Cha Mapinduzi wakati serikali ikielekea katika Uchaguzi Mkuu na kuwa ilani ilipaswa kuwa imetekelezwa kwa asilimia 100.
Waziri Mkuu alisema fedha zitakazotengwa katika mwaka wa fedha 2010/2011 zitakwenda kukamilisha utekelezaji wa ilani hiyo katika baadhi ya maeneo, kwani ndio mwaka wa tano wa Serikali ya Awamu ya Nne kukamilisha ahadi zake kwa mujibu wa ilani ya uchaguzi.
“Nataka niseme tu kwamba muda wa serikali kumalizia ahadi zake bado upo na hii bajeti ya mwaka 2010/2011 ndiyo bajeti yetu ya tano ambayo ndiyo itakayotuwezesha kukamilisha ahadi zetu zilizobaki,” alisema Pinda.
Tanzania Daima
My Take:
HIvi kweli hawa watu wanauchungu wowote na fedha za walipa kodi wa Tanzania?
Uhuru wa mbuzi zizini ni uhuru kwa kadiri ya kwamba chui hajasikia njaa - MM original
Bookmarks