+ Reply to Thread
Results 1 to 5 of 5

Thread: Ni msukumo upi unapelekea wimbi la vijana kugombea uongozi kupitia CCM?!

  1. #1

    Default Ni msukumo upi unapelekea wimbi la vijana kugombea uongozi kupitia CCM?!

    Vijana waliojitokeza kugombea nafasi za ubunge na uongozi katika ngazi nyinginezo kwa tiketi ya CCM ni wengi na wanazidi kuongezeka. Wengi wa vijana hawa ni wasomi na wenye shahada za juu kielimu, na baadhi yao wamebahatika kuishi nchi mbalimbali za ng'ambo na kujionea yaliyoko huko.

    Hatua wanazochukua kufanya hivyo ni haki yao na ni jambo la kupongezwa pale ambapo nia na malengo ni maendeleo ya Taifa letu. Lakini kwa kuwa wengi wao ni vijana walio elimika (nakujua vyanzo vya matatizo yetu), inakuwakuwaje wanagombea kupitia CCM? Nasema hivi kwani kitu kimojawapo ninachoamini kuwa ni kikwazo katika kuleta kasi ya maendeleo ya Taifa letu ndani ya mfumo wa vyama vingi ni kutokuwepo kwa uwakilishi wa kutosha wa upinzani, haswa katika ngazi ya ubunge.

    Basi nauliza:

    --- wakiwa ni vijana wasomi, nini kinawafanya waende CCM hali chama hicho kina wabunge wengi tayari tena wanaozidi wapinzani maradufu?

    --- je, hawaamini kuwa kuendeleza upinzani ni jambo la msingi kwa maendeleo ya Taifa letu?

    --- ni nini ambacho wanaweza kubadilisha wakiwa ndani ya CCM ambacho imeshindwa kukifanya mpaka leo hii kama chama tawala?

    --- wanahofia nini kuingia upinzani na kuundeleza wakiwa kama vijana wenye lengo la kuendeleza Taifa hili kwa nia njema kabisa huku wakiujenga mfumo wa vyama vingi?

    ---

    Steve Dii

  2. #2
    Join Date
    May 2010
    Location
    China
    Posts
    7

    Default

    Mkuu,
    Wengi wa hao vijana wasomi wanaoamua kuingia kwenye kugombania uongozi wa namna hiyo kupitia CCM si kwamba wamevutwa na dhamira safi ya kutaka kuwatumikia wananchi kama wengi wao wanavyodai. Wengi wao wapo kimaslahi zaidi na hivi wanadhani uhakika wa kuchaguliwa ili kufanikisha malengo ya kisiasa utapatikana kupitia CCM. Na siyo siri hali hii inawakumba hata wananchi wapiga kura wenyewe ambapo wanaoamini bado hakuna jambo jema litakaloweza kutoka nje ya CCM na hivi kutokuupa nguvu upinzani.

  3. #3

    Default

    Quote Originally Posted by monsignor View Post
    Mkuu,
    Wengi wa hao vijana wasomi wanaoamua kuingia kwenye kugombania uongozi wa namna hiyo kupitia CCM si kwamba wamevutwa na dhamira safi ya kutaka kuwatumikia wananchi kama wengi wao wanavyodai. Wengi wao wapo kimaslahi zaidi na hivi wanadhani uhakika wa kuchaguliwa ili kufanikisha malengo ya kisiasa utapatikana kupitia CCM. Na siyo siri hali hii inawakumba hata wananchi wapiga kura wenyewe ambapo wanaoamini bado hakuna jambo jema litakaloweza kutoka nje ya CCM na hivi kutokuupa nguvu upinzani.
    Kwa kweli inasikitisha...yaani unapoona jamii kwa mapana inaishiwa uwezo wa kung'amua yupi yu bora na yupi ni msaliti kutokana na shinikizo lililoundwa na kujijenga kwa manufaa ya wachache; hapo kunatatizo. Mifumo na mihimili yote inayosimamia uzima wa Taifa inakuwa imenajisiwa, haki kupotea na imani kutoweka.

  4. #4

    Default

    Opportunisms.

  5. #5
    Join Date
    Dec 2009
    Location
    Tanzania
    Posts
    240

    Default

    Quote Originally Posted by 911 View Post
    Opportunisms.
    Pamoja na ujinga.
    Follow the bee here

+ Reply to Thread

Thread Information

Users Browsing this Thread

There are currently 1 users browsing this thread. (0 members and 1 guests)

     

Similar Threads

  1. Malecela kugombea tena!
    By mwanakijiji in forum Siasa Za Tanzania/ Tanzanian Politics
    Replies: 2
    Last Post: 01-26-2010, 10:35 AM
  2. Kupinga Kikwete kugombea 2010 siyo uhaini!
    By mwanakijiji in forum Siasa Za Tanzania/ Tanzanian Politics
    Replies: 1
    Last Post: 12-22-2009, 08:51 PM
  3. Uongozi na Maendeleo - Sauti toka Ahera
    By mwanakijiji in forum Hoja
    Replies: 3
    Last Post: 10-16-2009, 10:31 PM
  4. Lowassa kurudishwa kwenye uongozi?
    By mwanakijiji in forum Siasa Za Tanzania/ Tanzanian Politics
    Replies: 5
    Last Post: 05-30-2009, 05:09 PM
  5. Mrema na Maalim Seif wastaafu Uongozi
    By dickabudi in forum Neutral
    Replies: 0
    Last Post: 03-24-2009, 11:26 AM

Bookmarks

Posting Permissions

  • You may not post new threads
  • You may not post replies
  • You may not post attachments
  • You may not edit your posts